CCM kugawa kadi za kielektroniki awamu ya pili

KATIBU wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Kenani Kihongosi amesema katika kuadhimisha miaka 49 ya kuzaliwa kwa CCM, chama hicho kitaaanza kugawa kadi za kielektroniki kwa wanachama wake kwa awamu ya pili.

Kihongosi amewasili Singida Mjini leo katika ziara yake ikiwa ni siku ya pili na kushiriki mkutano na wanachama wa Shina namba moja lililopo Kata ya Kindai.

Akizungumza na wananchama wa shina hilo Kihongosi, alisema CCM imepiga hatua katika matumizi ya Tehama hasa katika utoaji wa kadi za kielekroniki kwa wanachama wake ambazo tayari zimeshakamilika.



