Ukuaji Pato la Taifa kufikia asilimia 6.9

wa kukua kwa asilimia 5.9 mwaka 2025 na kuongezeka hadi asilimia 6.3 mwaka 2026 na asilimia 6.9 katika kipindi cha muda wa kati.
“Mfumuko wa bei kuwa kwenye wigo wa tarakimu moja ya wastani wa asilimia kati ya 3.0 – 5.0 katika muda wa kati.
“Mapato ya ndani kufikia asilimia 17.1 ya Pato la Taifa mwaka 2026/27 na wastani wa asilimia 17.1 katika kipindi cha muda wa kati.
“Mapato ya kodi kufikia asilimia 13.7 ya Pato la Taifa mwaka 2026/27; Kuhakikisha misamaha ya kodi haizidi asilimia moja ya Pato la Taifa.
“ Kuwa na nakisi ya bajeti isiyozidi asilimia 3.0 ya Pato la Taifa; na v kKuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango kinachokidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne,” amesema Waziri Mkumbo.



