Sh Tril 477 kugharamia Mpango wa Maendeleo

DODOMA; SERIKALI imesema gharama za utekelezaji wa Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano zinakadiriwa kuwa Sh trilioni 477.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof Kitila Mkumbo, ametoa kauli hiyo bungeni leo akiwasilisha nyenzo tatu zitakazowezesha kuanza utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Nyenzo hizo ni Mpango Elekezi wa Muda mrefu wa miaka 25 (2026/27 hadi 2050/51), Mpango wa Nne wa Maendeleo wa miaka mitano (2026/27 hadi 2030/31) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2026/27.

“Hiki ni kiasi cha fedha kitakachohitajika kuwekezwa katika sekta za kimageuzi na vichocheo vya ukuaji wa uchumi, ikiwemo usafiri fungamanishi; nishati na uchimbaji; viwanda na biashara; kilimo,TEHAMA; mazingira na uhimilivu wa tabianchi; huduma za kijamii na maendeleo ya watu; utawala na utumishi wa umma; pamoja na utafiti na maendeleo.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, vyanzo vikuu vya rasilimali za kugharamia Mpango huu ni sekta binafsi na sekta ya umma kwa uwiano wa 70:30.

“Sekta binafsi inatarajiwa kuwekeza takribani TZS trilioni 324.49 (70%), taasisi za serikali (MDAs na LGAs) zitachangia TZS trilioni 115.04 (22%), na Mashirika ya Umma (PSCs) yatawekeza TZS trilioni 38.22 (8%),” amesema Waziri Mkumbo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button