Mabadiliko sera za washirika kuathiri mpango na bejeti

DODOMA; SERIKALI imesema uchambuzi wa awali uliofanywa unaonesha kuwa utekelezaji wa mpango na bajeti ya Serikali kwa mwaka 2025/26 na muda wa kati unaweza kuathiriwa na mabadiliko ya sera za Washirika wa Maendeleo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha, Balozi Khamisi Mussa Omar akiwasilisha bungeni mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti ya serikali katika kipindi cha muda wa kati (2026/27 – 2028/29).
“Mnamo tarehe 27 Novemba 2025, Bunge la Umoja wa Ulaya liliazimia kuahirisha utoaji wa fedha za msaada kwa mikataba mipya ambayo serikali ilitarajia kuingia yenye thamani ya takribani EUR milioni 156, sawa na shilingi bilioni 445.75.
“Kwa mikataba inayoendelea, serikali inaweza kukosa misaada ya kibajeti kutoka Umoja wa Ulaya yenye thamani ya takribani EUR milioni 39.20, sawa na shilingi bilioni 113.8 kwa mwaka 2025/26 na shilingi bilioni 27.2 kwa mwaka 2026/27. 21.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi nyingine iliyotoa tamko la kusitisha misaada ni Sweden ambapo imesitisha kutoa SEK 119,552,997, sawa na shilingi bilioni 31 kwa ajili ya programu ya elimu ya EpforR kwa mwaka 2025/26 baada ya kulazimika kuongeza misaada zaidi kwa nchi ya Ukraine iliyoathiriwa na mgogoro wa kivita kati yake na Urusi.
“Miongoni mwa mikakati ya Serikali ya kukabiliana na mabadiliko haya ni kuendelea kuongeza jitihada za ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuwianisha mapato na matumizi, pamoja na kutoa kipaumbele kwa mahitaji ya msingi ikiwemo mishahara, deni la Serikali na huduma za jamii,” amesema Waziri wa Fedha.




Loved reading this well-researched article.
The website is genuinely helpful and worth bookmarking.