Jamii yatakiwa kuzingatia unyonyeshaji sahihi

MTWARA: JAMII mkoani Mtwara imetakiwa kuhakikisha watoto wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kuchanganya na kitu chochote ili aweze kupata mkuzi sahihi.
Hayo yamejiri wakati wa kikoa cha wadau mbalimbali mkoani humo wakiwemo asasi za kiraia cha robo mwaka kuhusu kufanya tathmini ya shughuli zilizofanyika kuanzia Oktoba mpaka Desemba 2025.
Pia mipango kazi ya kuanzia Januari mpaka Machi 2026 kupitia Program Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) kikao ambacho kimefanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani humo.
Meneja Mradi kutoka Taasisi isiyo ya Kiserikali mkoani humo ya KIMAS Torai Kibiti amesema katika baadhi ya maeneo ambayo yameonesha bado kuwa na changamoto ikiwemo hilo la kuona watoto wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kuchanganya na kitu chochote.

‘’Kiashiria cha kuonyesha kwamba hamasa inatolewa kiko vizuri na akina amama wanapata elimu lakini sasa utekelezaji wa kuonesha kwamba akina mama wangapi wananyonyesha maziwa pekee bila kuchanganya bado tuko chini’’amesema Torai
Amesema bado wana kazi kubwa ya kufanya katika eneo hilo kwasababu ni swala tu la uelewa kutokana na watu wanaamini kwamba mtoto ambaye hajafikisha miezi sita haiwezekani akanyonya maziwa ya mama pekee hivyo wamekubaliana waongeze hamasa kwenye jamii hiyo.
Mwakilishi wa Kituo cha Msaada wa Kisheria cha Nerio kwenye manispaa hiyo Judith Chitanda amesema makuzi, malezi na maendeleo ya awali ya mtoto ni kuanzia umri wa mwaka 0 hadi miaka 8 ambapo kikubwa walichokiangalia ni wanavyoweza kupata maendeleo yao katika sekta mbalimbali ikiwemo afya ambako mtoto anatakiwa kunyonyeshwa vizuri ili kupata makuzi sahihi.
Akiwasilisha mada kuhusu chombo kinachotumika kupima hali ya utekelezaji na ubora wa utoaji wa huduma za makuzi, malezi na maendeleo ya awali ya mtoto (Scorecard),
Kwa niaba ya Ofisa Ustawi Mkoa wa Mtwara, Ofisa Ustawi wa manispaa hiyo Godlove Miho amesema moja ya faida ya chombo hicho ni kusaidia kujua ubora wao wa utaoji huduma kwa watoto.



