Ujenzi wa Daraja Mto Pangani wafikia asilimia 80

DODOMA; Serikali imesema inatekeleza ujenzi wa Barabara ya Tanga – Pangani – Saadani hadi Makurunge (km 256) kwa kiwango cha lami kwa awamu nne.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya, amesema hayo leo bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tanga Mjini, Kassim Mbaraka aliyetaka kujua lini serikali itakamilisha ujenzi wa barabara ya Tanga – Pangani – Saadani hadi Makurunge kwa kiwango cha lami.
“Serikali inatekeleza ujenzi wa barabara ya Tanga – Pangani – Saadani hadi Makurunge (km 256) kwa kiwango cha lami kwa awamu nne.
“Awamu ya kwanza ni ujenzi wa barabara ya Tanga – Pangani (Km 50), ambao umefikia asilimia 77. Awamu ya pili ni ujenzi wa Daraja la Mto Pangani pamoja na barabara unganishi (km 14) ambapo ujenzi umefikia asilimia 80.16.
“Awamu ya tatu ni ujenzi wa barabara ya Tungamaa – Mkwaja – Kwamsisi – Mkange (km 92.5), ujenzi wake umefikia asilimia 57.38).
“Aidha, sehemu ya nne iliyobaki ya Mkange – Makurunge (km 75) usanifu umekamilika na Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kuanza ujenzi wa barabara hiyo,” amesema Naibu Waziri huy

