Maeneo yanayofaa mradi umeme wa upepo, jua yatajwa

DODOMA; SERIKALI imesema kupitia Sera ya Taifa ya Nishati ya mwaka 2015, imeweka mkazo wa kuendeleza vyanzo vya nishati jadidifu hususan upepo na jua, ili kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na nafuu kupitia vyanzo mbalimbali.
Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba ametoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mwera, aliyehoji serikali ina mpango gani wa kutumia vyanzo vya umeme vya upepo na jua vilivyopo nchini.
‘’Katika kutimiza azma hii, serikali imekwishabainisha na kufanya utafiti wa maeneo mbalimbali yanayofaa kuendelezwa kwa miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia upepo na jua, ikiwa ni pamoja na Zuzu – Dodoma, Same – Kilimanjaro na Manyoni – Singida na uendelezaji wa maeneo hayo kwa kushirikiana na sekta binafsi upo katika hatua mbalimbali.
‘’Kwa sasa serikali inatekeleza mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 150 katika Wilaya ya Kishapu, Shinyanga ambapo awamu ya kwanza ya mradi huo yenye megawati 50 imekamilika na hatua za kuingiza umeme huo katika Gridi ya Taifa zimeanza.
‘’Katika hatua za kuboresha mazingira ya uwekezaji wa sekta binafsi katika vyanzo vya nishati jadidifu (jua, upepo, jotoardhi na vyanzo vingine), serikali ipo katika hatua za mwisho za kuboresha mikataba kifani ya kuzalisha na kuuziana umeme,” amesema.


I earned $17,932 last month by working online for just 2 hours a day. This job is simple, flexible, and beginner-friendly,S1 making it accessible to everyone. It has helped me manage my finances effortlessly while focusing on my education as a full-time student.
You can click on this the website and begin
right away….www.today.earn54.com