Fountain Gate kuendeleza heshima ya soka Arusha

ARUSHA: UONGOZI wa timu ya Fountain Gate FC umeeleza kuendeleza heshima ya soka mkoani Arusha kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwa kuwa na historia ya timu kushiriki ligi kuu kutokana na kuweka makazi yake mkoani humo.

Timu ya Fountain Gate FC imehamia rasmi mkoani Arusha ikitokea Manyara yalikokuwa maskani yao na kupokelewa kishujaa huku uwanja wa nyumbani katika michezo ya ligi kuu ya NBC Tanzania utakuwa Sheikh Amri Abeid huku wakitatambulika kama ‘Chuga boys ‘Chama la watalii’ ikiwa chini ya mlezi wake Mkuu wa Mkoa Arusha CPA Amos Makalla

Akizungumza katika hafla ya mapokezi kwa timu hiyo, Mkurugenzi wa Fountain Gate Japhet Makau ameeleza kuwa wamekuja Arusha kuuheshimisha Mkoa ikiwa ni moja ya mikoa maarufu yenye vivutio vingi vya utalii lakini katika historia ya soka umekuwa na Mafanikio makubwa .

“Arusha imekuwa na mafanikio mengi katika soka miaka ya nyuma na sio mkoa ambao unastahili kutokuwa na timu ya ligi kuu, wale wa siku nyingi wanatambua uwepo wa timu ya Ndovu, AICC,Palson AFC hizi ni klabu ambazo zilikuwa tishio katika ligi kuu ya Tanzania na tumekuja kuhakikisha tunaendeleza ile heshima kama ilivyoanzishwa na wazee wetu wa siku nyingi,” amesema Makau.

Amesema Mkoa wa Arusha umekuwa na heshima kubwa ya wachezaji maarufu kama Muhidin Cheupe na wengine wengi.

“Fountain Gate iko tayari na iko vizuri na mwaka huu tumefanya usajili mzuri baada ya kupata changamoto katika msimu uliopita mwaka huu tumetengeneza jeshi ambalo linakwenda kupigana vizuri,lina mchanganyiko wa wachezaji wenye uzoefu katika ligi ya Tanzania na pia kutoka nje,”amesema Makau.

Mkuu wa Mkoa Arusha, CPA Amos Makalla amesema Arusha ni mkoa mkubwa wa utalii hivyo uwepo wa timu hiyo utaongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi wake.
Ikiwa ni pamoja na utalii wa michezo .

“Nawakaribisha Arusha,nimewapokea na niwaombe wananchi muipokee kwani faida ya kuwa na timu hii ni kubwa mno kuna Utalii na Utalii wa michezo maana yake Fountain wakiwa hapa timu zote za ligi kuu zitakuja hapa hivyo kuongeza zaidi fursa kwani bodaboda atafaidika, mamantilie, masoko na hoteli kwa hiyo mnyororo wa thamani unawagusa wana Arusha wote hivyo timu za Simba,Yanga, Azam , Singida na nyingine zikija watu watafurahi ,” amesema Makalla.

Amewasihi Wadau wa michezo makampuni kuwekeza na kufanya kazi na Fountain Gate, na kusema mkoa huo una wadau wengi na wana kiu ya michezo na uwepo wao ni chachu katika kuelekea michuano ya AFCON 2027.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…
    Try it, you won’t regret it!….. http://www.hot.cash54.com

  2. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com

  3. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button