Malengo ya JKT Marathon yaleta mafanikio kwa jamii

DODOMA: Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud amesema SUMA JKT Marathon imefanikiwa kufikia malengo yake makuu matatu ya kuchangia huduma za afya, kutangaza bidhaa zinazozalishwa na JKT pamoja na kutoa fursa kwa wajasiriamali kuonesha na kuuza bidhaa zao.

Naibu Waziri amesema hayo katika Maadhimisho ya Kilele cha Mbio hizo leo 7, Juni 2026 jijini Dodoma ambapo A
amesema mbio hizo pia zimeimarisha uhusiano kati ya wananchi na jeshi hilo kwa kuendeleza uzalendo na mshikamano katika kujenga taifa.

Naye, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali John Jacob Mkunda amesema JKT Marathon imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi kwa kuhamasisha mazoezi na afya njema, kujenga mahusiano na kuimarisha mshikamano.

Kadhalika amebaisha kuwa mbio hizo zimefanikiwa kuchangisha zaidi ya Shilingi milioni 160 zilizotolewa kwa Hospitali ya Makole na Hospitali ya Jeshi iliyopo Mwenge jijini Dar Es Salaam ili kusaidia kuboresha huduma za afya.

Kwa upande wake, Kocha wa timu ya Riadha ya Majeshi Tanzania, Antony Muingereza ameipongeza JKT kwa kuendelea kuandaa mashindano yanayochochea maendeleo ya riadha nchini na kutoa wito kwa Serikali na sekta binafsi kuongeza udhamini katika mchezo huo.

Ameongeza kwa uwekezaji katika riadha unasaidia kukuza vipaji vya wanariadha na kutoa fursa kwa wadhamini kutangaza taasisi na bidhaa zao ndani na nje ya nchi

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button