Serikali yajizatiti uwekezaji miradi ya maendeleo

DAR ES SALAAM: Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amesema serikali inaendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika miradi ya maendeleo yenye lengo la kuboresha maisha ya Watanzania.

Dk Jafar Seif ameyasema hayo Febuari 7 wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya katika Kata za Buguruni na Kimanga, jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika Kata ya Buguruni, Naibu Waziri ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha zoezi la ulipaji fidia kwa nyumba nane zitakazopisha ujenzi wa kituo cha afya linakamilika kwa haraka ili kuruhusu mradi huo kuanza kutekelezwa bila kuchelewa.

Katika Kata ya Kimanga, Dk Jafar Seif ameagiza ujenzi wa kituo cha afya kuanza mara moja baada ya Serikali kutenga kiasi cha Sh milioni 140 kama fedha za awali kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Segerea, Agnesta Lambert Kaiza, ameishukuru serikali ya Rais Samia kwa kuonyesha dhamira ya dhati ya kuwahudumia wananchi wa jimbo hilo, huku akisisitiza umuhimu wa utekelezaji wa haraka wa maagizo yaliyotolewa.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema ziara ya Naibu Waziri ni uthibitisho wa utekelezaji wa ahadi za Serikali ya Awamu ya Sita, akieleza kuwa Serikali ya Rais Samia inaendelea kusimamia kwa vitendo miradi inayolenga ustawi wa wananchi.





I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com