Waliodhalilishwa kijinsia kuwezeshwa kiuchumi

ZAIDI ya wanawake 60 waliokumbwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo ukatili wa kijinsia, wanatarajiwa kupatiwa mafunzo ya urembo bure ikiwa ni hatua ya kuwainua na kuwawezesha kiuchumi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho cha urembo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke na Uongozi (WnU), Shamira Mshangama, amesema ili kufanikisha hilo wamezindua rasmi saluni iitwayo Mwanamke na Uongozi Saluni, itakayotoa mafunzo ya urembo wa nywele, kucha na vipodozi (make-up) bure kwa muda wa miaka miwili.

“Tunawawezesha wanawake kushiriki katika nafasi za maamuzi na uongozi. Leo tunazindua Mwanamke na Uongozi Saluni. Tangu mwaka 2017 tulipoanza, tuligundua changamoto za ukatili ambazo wasichana wanapitia, na sababu kubwa ni ukosefu wa kipato binafsi. Kwa kushirikiana na mfadhili wetu, Women First International Fund, tumeanzisha mradi huu,” amesema.

Amesema mradi huo unaitwa ‘Nafasi ya Kuanza Upya’, ambapo watatoa mafunzo ya urembo bure kwa lengo la kuwawezesha wanawake kujipatia kipato binafsi. Pia amesema taasisi hiyo itatoa ajira katika ofisi yake, huku walengwa wakuu wakiwa ni wanawake wanaopitia changamoto za kijinsia.

“Tunataka kuhakikisha wasichana wengi wanapata mafunzo. Hiki kitakuwa kituo cha mafunzo kwa wasichana kujifunza urembo. Pia taasisi itajipatia kipato kitakachoiwezesha kuwafikia mabinti wengi zaidi kupitia miradi ya kuwainua kiuchumi,” ameongeza.

Kwa upande wake, mfanyakazi wa kitengo cha saluni, Sauda Milidadi, amesema kabla ya kufika hapo alipitia changamoto ya kumlea mtoto wake peke yake, lakini baada ya kupata mafunzo na ajira, ameweza kujihudumia yeye na mtoto wake. SOMA: Ukatili wa Kijinsia Unaendelea Kuathiri Jamii

“Nina mtoto mmoja ninamlea peke yangu. Nilifika hapa nikapata kazi na hadi sasa bado niko hapa. Mabinti wengi kwenye kazi ni wagumu kujitoa. Tujitoe kwa moyo mmoja, tupambane kupata kipato chetu binafsi. Wajitokeze, taasisi inasaidia sana na tutatatua changamoto kwa pamoja,” amesisitiza.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..  www.join.work27.com 

  2. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..  www.join.work27.com 

  3. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do……………………………………………………………………………………..
    ………………………………………………………  www.join.work27.com 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button