Tutumie Siku ya Wapendanao kuwakumbuka wahitaji

SIKU ya Wapendanao Februari 14 ambayo kwa Kiingereza huitwa ‘Valentine’s Day’ ni siku ambayo watu wengi kuipa hadhi ya mapendo na kuisherehekea maeneo mbalimbali duniani. Historia ya siku hii ilianzia Karne ya 3 huko Roma wakati wa utawala wa Claudius wa II kupitia Padri Valentinus (Valentine) ambaye alikuja kuheshimiwa kama mtakatifu, hasa kwenye tarehe hiyo.
Siku hii ilianzishwa maalumu na Papa Gelasius kama kumbukumbu ya kifo cha Mtakatifu Valentine wa Roma ambaye aliuawa Februari 14 baada ya kuhukumiwa kifo, kutokana na kuhubiri injili iliyohamasisha vijana kuacha kuishi maisha ya uasherati na kufunga ndoa, kitendo ambacho hakikuwa kikiruhusiwa na watawala kwa wakati huo kwa kuwa walitaka vijana waingie jeshi bila kuoa.
Inasemekana Valentine alikuwa akifanya matendo mengi ya upendo kwa watu wote, ikiwamo kuwafungisha ndoa wanajeshi ambao hawakuwa wakiruhisiwa kufanya hivyo. Hii ilisababisha kukamatwa na kufungwa gerezani. Pia, alimuombea binti aliyekuwa na tatizo la kutokuona, akaona na akawa anamtembelea gerezani. Kabla ya kuuawa, Valentine alimuandikia binti huyo barua ambapo mwishoni aliweka sahihi inayosema “Your Valentine” yaani ‘Valentine Wako’ ili iwe kumbukumbu yake kwake.
Baada ya kifo cha Valentine na kupita kwa karne kadhaa, Karne ya 14 na 15 siku hii ya Februari 14 ikaanza kuhusishwa na mapenzi na kusherehekewa maeneo mengi duniani kama ishara ya kuunganisha upendo kwa familia, wanandoa, ndugu na jamaa kumuenzi Valentine.
Kulingana na miaka inavyozidi kwenda, siku hii imekuwa ikiendelea kujizolea umaarufu mkubwa kwani wapenzi wamekuwa wakiisheherekea kwa namna tofauti na kuoneshana ni kwa namna gani wanapendana, ikiwamo kupeana zawadi. Katika baadhi ya maeneo, watu hutumia siku hii kunogesha mahusiano yao kwa kupeana zawadi na wengine wameenda mbali kwa kuchagua siku hii kama siku ya kipekee ya kufunga ndoa au familia kukaa pamoja.
Hata hivyo, yapo mahusiano yanayovunjika siku hii au kugeuka shubiri kutokana tu na wapenzi kutoambiana nakupenda au kutopewa zawadi. Lakini wapo wengine ambao huitumia siku hii kuwapa zawadi wazazi, walezi, dada, kaka au watoto wao ikiwa ni ishara ya kuonesha thamani yao na namna wanavyowapenda, kuwajali na kuwahitaji maishani.
Binafsi natamani ili siku hii ilete maana ya upendo, tuitumie kuwathamini watu wenye mahitaji kwa kuwatembelea hasa yatima, wazee na wale wasiojiweza na kuwapa mahitaji mbalimbali kadiri Mungu atakavyotujalia.Tukifanya hivyo, tutaongeza thamani maishani mwao na kujiona na wao ni binadamu kama wengine na wanapendwa.
Nashauri tutumie siku hii kuwa sehemu ya watatuzi wa changamoto za wengine kama mavazi, chakula, matibabu, elimu, malazi ili kuweka maana ya upendo katika maisha yao na kumgusa Mungu kupitia wao. Naamini kufanya hivyo pia ni moja ya sadaka njema na maandiko yanaeleza watu anayesadia wahitaji, atazidi kubarikiwa. SOMA: Bella, El Saadat, Twanga Pepeta kukiwasha Valentine Day
Nashauri tusitumie muda mwingi kuweka nguvu ya kumfurahisha mpenzi, mwenza Februari 14 kila mwaka kama vile siku nyingine hamfurahiani, bali muupe thamani upendo kwa kuwafurahisha wahitaji na hii ina tija zaidi. Suala la kuoneshana mapenzi, kuambiana ninakupenda na kupeana zawadi linapaswa kuwa la mara kwa mara ili kudumisha pendo. Pia, hili linahusu wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki pia na si wapenzi wenye ndoa peke yao. Nawatakia heri ya Siku ya Wapendanao.




My best friend’s sister gets $180 an hour on the internet… she’s been laid off for two months, the previous month her paycheck was $20328 only working at home for a couple of hours each day…
check out……… http://www.jobathome1.com