Malima ataka uwajibikaji changamoto za wanawake

MOROGORO: MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amewaagiza  watendaji wa mitaa, vijiji na kata za mkoa huo kushughulikia kikamilifu migogoro ya ardhi inayowakabili wanawake wanaponyang’anywa umiliki baada ya wanaume wao kufariki au kutengena pamoja na kudhibiti unyanyasaji wa kijinsia

Malima ametoa agizo hilo katika hotuba yake kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoanzimishwa kimkoa katika kijiji cha Fulwe,kata ya Mikese, Wilaya ya Morogoro Machi 8, 2026.

Mkuu wa mkoa amesema kwa watendaji wa ngazi hizo ambao watashindwa kutekeleza majumumu yao ipasavyo ya kusimamia utoaji haki kwa wanawake wenye kudhurumiwa hazi zao watajihesabu wameshindwa kazi nawanapaswa wajiengue wenyewe.

Pamoja na hayo aliwataka wanawake wanapokuwa wananyanyaswa na  kunyang’anywa mali walizochuma nawaume zao wasisite kuchukua hatua za kuwasilisha malalamiko yao kwenye vyombo vya utoaji wa haki ikiwemo mahakamani.

“Wanawake msisubiri mambo yanawaharibikia, hamyasemi hadi mnaponyang’anywa mali  pale mume anapofariki dunia, jitokeze mapema kwenye chombo cha sheria,”amesema Malima.

Malima amewataka wenye kupatwa na kadhia hizo wasisite kutumia haki zao kwenda mahakamani na katika madawati wa jinsia ya Polisi kuweza  kupata msaada wa kisheria na kupata haki zao.

“Kuna hili dawati maalumu la jinsia la Polisi, na limekuwa na nguvu, ninalipongeza dawati hili la jinsia limefanya kazi nzuri , dawati limesaidia kuleta mabadiliko makubwa kwa watu wanaoleta kesi na zimekuwa zikiongezeka na kufanyiwa kazi,” amesema Malima.

Mkuu wa mkoa alilitaka dawati la jinsia la Polisi kuendelea kufanya kazi ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na Watoto ndani ya mkoa wa Morogoro.

Pia aliwataka wanawake kuangalia nafasi zao kwa kuendelesa  kuongeza kasi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi ili kuliwezesha Taifa kusonga mbele.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Morogoro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,Sheila Lukuba alisema atahakisha anafuatilia mikopo ya asilimia kumi inayotengwa na halmashauri za mkoa huo kuona inatolewa Kwenda kwa  walengwa (vikundi ).

Mbunge huyo pia amesema Rais Dk Samia Suluhu Hassan alishaoa fedha zaidi ya Sh bilioni mbili kupitia Ahadi yake ya siku 100 baada ya kuapisha awamu ya pili kipindi cha pili ya uongozi wake kua anazitoa fedha hizo na tayari zimetolewa .

“Fesha hizo zimetolewa na fursa hii ipo , niwaombe wafanyabiashara wadogo  , mama lishe na bodaboda wachangamkie fursa kwa kuchukua mikopo,” amesema Sheila.

Sheila pia amewasisitiza wazazi hususani wanawake kuhakikisha wanasimamia vyema watoto wao katika elimu kwani elimu inatolewa bila malipo kuanzia msngi hadi sekondari.

Mbali na hayo amesema kwa nafasi yake anawajibu wa kuwatetea wanawake wote wanaonyanyasika kwa kutumia madawati ya jinsia ya polisi na kwa kuwatumia maofisa ustawi wa jamii ambao wapo kwenye halmashauri zote tisa za mkoa huo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button