Kamati ya Bunge yapongeza huduma za mama na mtoto

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI imetoa maelekezo kwa hospitali zote nchini kufuata miongozo ya Bunge katika kuimarisha programu za afya ya mama na mtoto.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati kamati hiyo ilipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Amana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk Johanes Lukumay, ameipongeza hospitali hiyo kwa kuimarisha huduma kwa watoto wachanga kupitia ubunifu wa mbinu za kuwatunza watoto njiti.
“Nimefurahi sana kuona wodi ya watoto njiti ilivyoandaliwa vizuri katika hospitali hii. Sera ya sasa inasisitiza utaratibu unaoitwa Zero Separation, yaani mtoto anapozaliwa anapaswa kuwa karibu sana na mama yake,” amesema Dk Lukumay.
Ameongeza kuwa hospitali hiyo pia inatumia mbinu ya Kangaroo Mother Care, ambapo mtoto huwekwa karibu na kifua cha mama yake ili kusaidia kuimarisha afya ya mtoto na kupunguza vifo vya watoto wachanga. Dk Lukumay amesema hospitali hiyo imepiga hatua zaidi kwa kuanzisha ubunifu unaoitwa Kangaroo Father Care, ambapo baba naye hushiriki katika kumlea mtoto kwa kumweka karibu na kifua chake.
Amesema hatua hiyo husaidia hasa pale mama anapojifungua watoto zaidi ya mmoja, kama mapacha au zaidi, ambapo baba anaweza kusaidia kumhudumia mmoja wa watoto. “Hii ni hatua kubwa sana. Ningependa hospitali nyingine nchini ziige mfano huu, kwani baba anapomshika mtoto karibu na kifua chake humsaidia pia mama kupata utulivu wa kisaikolojia na kuongeza uzalishaji wa maziwa, jambo linaloimarisha afya ya mtoto,” amesema.
Aidha, ameipongeza Serikali kwa hatua ya utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, ambayo itaanza kutekelezwa nchini kote na kuwezesha watoto chini ya miaka mitano kupata huduma za afya bila malipo. “Katika mfumo huu wa bima, wanawake wajawazito watapata huduma bila malipo, wazee wetu watapata huduma bila malipo na kaya maskini nazo zitahakikishiwa kupata huduma bora za afya bila malipo,” amesema.

Kamati hiyo pia imeitaka Wizara ya Afya kuangalia namna ya kuongeza watumishi katika hospitali hiyo ili kuboresha zaidi huduma kwa wagonjwa. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Dk Florence Samizi, amesema wamepokea maelekezo ya kamati hiyo, hususan kuhusu uhaba wa wauguzi.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan aliahidi kuajiri watumishi wa afya 5,000 na kwamba mchakato wa kuwasambaza watumishi hao unaendelea nchini kote. “Tunaendelea kushirikiana na mamlaka husika kuhakikisha wauguzi zaidi wanapelekwa katika Hospitali ya Amana, hasa katika wodi ya watoto wachanga,” amesema.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Amana, Dk Brayson Kimweri, ameishukuru kamati hiyo kwa kuitembelea hospitali hiyo na kuahidi kuzingatia pamoja na kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa. SOMA: Samia ang’ara afya ya Mama na Mtoto




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com