Kamati yataka kasi uboreshaji Bandari ya Tanga

TANGA: KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeitaka Serikali kuharakisha utatuzi wa changamoto za miundombinu wezeshi katika Bandari ya Tanga, ili kuendana na kasi ya ongezeko la meli kubwa na shehena inayopokelewa bandarini hapo kwa sasa.
Hayo yamebainishwa leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Joyce Ndalichako, wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utendaji na ufanisi wa bandari hiyo, ambayo imetajwa kuwa mbadala muhimu katika kupunguza msongamano wa mizigo kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kukagua gati jipya, Profesa Ndalichako amesisitiza kuwa maboresho ya bandari pekee hayatoshi ikiwa miundombinu ya usafirishaji inayounganisha bandari hiyo na maeneo mengine haitaimarishwa.
“Kamati inasisitiza kuwa ni muhimu kasi ya ujenzi wa barabara za kuingia na kutoka bandarini sambamba na reli ziboreshwe. Hii itarahisisha usafirishaji wa mizigo kwenda kwa walaji kwa wakati,” alisema Profesa Ndalichako.

Pongezi kwa Rais Samia Mwenyekiti huyo alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, kwa maono yake ya kuifungua Tanga kiuchumi.
Alibainisha kuwa mpango wa kuunganisha bandari hiyo na reli ya kisasa ya SGR kuelekea Musoma utakuwa mkombozi wa ajira na tija kwa taifa.
Mikakati ya Serikali (Reli ya SGR)
Akifafanua kuhusu hatua zinazochukuliwa, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, amesema Serikali tayari iko kazini kuunganisha bandari hiyo na mtandao wa reli wa kilomita 248 (Tanga–Mruazi–Ruvu) kuelekea Arusha.

Aidha, Kihenzile aliongeza kuwa mradi wa SGR utakaopita Minjingu na Engaruka hadi Musoma utakuwa kiungo muhimu cha kibiashara kwa nchi za maziwa makuu na maeneo ya kaskazini mwa nchi.
Kwa upande wake, Meneja wa Bandari ya Tanga, Salehe Mbega, amesema maboresho makubwa yamefanyika ikiwemo kuongeza kina cha maji kufikia mita 12.

Hatua hiyo imewezesha meli kubwa zenye urefu wa hadi mita 200 kutia nanga, jambo ambalo halikuwezekana hapo awali.
Hata hivyo, Mbega amebainisha kuwa kutokana na ubora wa huduma, mahitaji yamekuwa makubwa kiasi cha kusababisha msongamano wa meli nje ya bandari.
Takwimu za Ufanisi kwa sasa:
Muda wa kuhudumia meli: Siku 3 hadi 5.
Meli zinazosubiri: Wakati mwingine hadi meli 14 hukaa nje ya bandari kusubiri huduma.
Mpango wa ujenzi wa magati matatu mapya na kituo cha kisasa cha abiria (Terminal) katika awamu ya tatu ya mradi.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com