‘Kill Marathon’ watoa taarifa barabara zitazotumika Machi 22

DAR ES SALAAM: WANDAAJI wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager wametoa taarifa kuhusu kufungwa kwa barabara zitakazotumika siku ya mbio hizo ambazo zimebaki wiki moja kabla ya kufanyika.
Taarifa iliyotolewa na waandaaji hao imesema kuwa taarifa hiyo itawasaidia wakazi wa Moshi na wageni kupanga safari zao mapema au kutumia njia mbadala wakati barabara zilizoainishwa zitakapofungwa siku ya mbio hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika Machi 22, 2026.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Barabara ya Sokoine kutoka kona ya KCMC hadi Barabara ya Kilimanjaro itafungwa kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 3:30 asubuhi.
Madereva wanashauriwa kutumia njia mbadala ambayo ni ya Shanty town na ile ya Rau ambayo zinaelekea hadi hadi Moshi mjini; wale wanaokwenda Mweka pia wanaweza kutumia njia hizo mbili, kupitia Shanty Town na Rau, na Pia barabara ya Kilimanjaro kwa kutokea kona ya Barabara ya Kilimanjaro na Barabara ya Sokoine itafungwa kuanzia saa 1:45 asubuhi hadi saa 9:30 asubuhi.
“Hii itawaruhusu wakimbiaji kufika kwenye maegesho yaliyoko kwenye shule ya polisi (TPS/CCP) na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) kwa upande wa lango lililoko barabara ya Uru ili kutoa nafasi kwa mbo hizo kuanza sambamba na kutoa nafasi kwa washiriki wa mbio hizo kukimbia bila wasiwasi,” imeeleza taarifa hiyo.
Taarifa ya waandaaji hao imendelea kusema kuwa Barabara ya Masoka hadi Mweka kupitia Kibosho pia itafungwa pande zote mbili kuanzia saa 12:30 asubuhi hadi saa 2:30 asubuhi, ambapo zile za kupitia Moshi Klabu hadi Weru Weru kupitia daraja la zamani na klabu ya Wessa zitafungwa kuanzia eneo la barabara ya Lema hadi kona ya Glacier saa 1:15 asubuhi hadi saa 3:15 asubuhi.
“Barabara zote zitakuwa chini ya udhibiti makini wa askari wa usalama barabarani haswa maeneo ya barabara ya Umbwe, kwenye vivuko vyote hadi sehemu ambayo wakiambiaji watageukia kuendelea na mbio hizo”, ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa hakutakuwa na maegesho katika Barabara ya Sokoine kutokea kona ya Barabara ya Kilimanjaro na kwamba magari yakayoegeshwa katika eneo hilo yatachukuliwa na polisi.
“Kutakuwa na maegesho ya bure katika eneo la shule ya polisi Tanzania lililoko kwenye barabara ya Barabara ya Kilimanjaro na lango la kuingilia watembea kwa miguu mahali ambapo mbio za Yas Half Marathon zitaanzia”,ilisema taarifa hiyo.
Pia kutakuwa na maegesho ya bure yenye kivuli katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika cha Moshi (MoCU) ambayo yatafikiwa kupitia Barabara ya Uru pekee, ambayo ni umbali wa dakika 5 kwa miguu hadi eneo ambalo mbio za Kimataifa za Half Marathon za Yas Kili na zile za kufurahisha za 5km (CRDB fun run) na pia ni dakika 2 tu kutoka eneo ambalo mbio za kilomita 42 za Kilimanjaro Premium Lager zitaanzia.
“Maofisa wa usalama barabara kutoka jeshi la Polisi watadhibiti njia zote zitakazotumika kuanzia majira ya saa 12 asubuhi had saa 6:30 mchana; madereva wanaombwa kuendesha polepole na kwa uangalifu na kuwa makini ili kuwalinda washiriki wa mbio hizo”, iliendelea kusema taarifa ya wandaaji, ambapo pia walitoa wito kwa madereva kuepuka kutumia njia zilizoainishwa ili kuepuka adha ya kusimamishwa kwa mdua mrefu ili kupisha wakimbiaji.
Aidha waandaaji pia walionya kuwa madereva wakiwemo wale wa boda boda watakaobainika kutumia mwendo wa hatari watachuliwa hatua za kisheria ambapo pia walitioa rai kwa wakimbiaji kuwa makini wakati wanashiriki mbio hizo.
Kuhusu maeneo ya ambayo vyombo vya usafiri wa abiria vitapakia au kushushia wasafiri taarifa hiyo imesema kuwa magari hayo yanaweza kushushia abiria kwenye maegesho yaliyotengwa kwa mujibu wa taratibu au kandokando ya barabara ilimradi iwe ni salama kwa abiria hao kupakia au kushuka kwenye usafiri husika.
Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa hakutakuwa na njia ya kufikia MoCU kutoka Barabara ya Sokoine kuanzia saa 12 asubuhi kwa hivyo wale wanaotarajia kushiriki mbio hizo watalazimika kushukia upande wa kona ya Barabara ya Sokoine, ambapo wanakumbushwa kuhakikisha wana muda wa kutosha kufika kwenye sehemu ambazo mbio zitaanzia.
Wakati huo huo, zoezi la ukusanyaji wa namba za ushiriki linatarajiwa kuanza Ijumaa ya tarehe 13 Machi, 2026 katika duka la Mlimani City (mbele ya Samaki Samaki) kuanzia saa 10 alasiri hadi saa 1 ya jioni, Jumamosi tarehe 14 Machi, 2026, kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni na Jumapili tarehe 15 Machi, 2026, kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni.
Baada ya Dar es Salaam, zoezi hilo litahamia Arusha siku ya Jumanne tarehe 17 Machi, 2026 na Jumatano tarehe 18 Machi, 2026, kuanzia saa 8 mchana hadi saa 1, katika Hoteli ya Kibo Palace.
Sehemu ya mwisho ya ukusanyaji itakuwa Moshi, kuanzia siku ya Alhamisi tarehe 19 Machi,2026, kuanzia saa 6 mchana hadi saa 11 jioni, Ijumaa tarehe 20 Machi, 2026, kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni na Jumamosi tarehe 21 Machi, 2026, kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 11 jioni, katika Uwanja wa MoCU.
Kwa mujibu wa waandaaji hao, idadi ya tiketi kwa ajili ya ushiriki wa mbio za CRDB 5Km bado zinapatikana na zitauzwa kwa fedha taslimu ambapo huduma zitatolewa kwa yule anaefika kanza kuhdumiwa kwanza, ambapo wanaotarajia kushiriki mbio za kipengele hicho wametakiwa kuchangamkia fursa hiyo kwa viel tiketi zilizobaki ni chache.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com
I get paid more than $90 to $120 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
This is what I do…. www.work27.online