CCM yatoa neno mradi wa umwagiliaji Mgambalenga

IRINGA: KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi amegiza kusiwe na pngezeko la muda wa kutekeleza mradi wa Umwagiliaji wa Mgambalenga ili wakulima waanze kunufaika nao.

Kihongosi ametoa agizo hilo leo Juni 18,2026 alipotembelea na kukagua utekelezaji w amradi huo unaojengwa katika Kijiji cha Mtandika, Kata ya Ruaha Mbuyuni Kilolo mkoani Iringa unaogharimu zaidi ya Sh bilioni 23.9.

Akizungumza hayo Kihongosi amesema mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2025 na ulitakiwa kukamilika mwaka 2025 lakini ulipelekewa mbele hadi 2026 na baadaye 2027 kutokana na changamoto zilizoelezwa kukwamisha utekelezaji, hivyo aliwataka watekeleza ndani ya muda huo.

“Matamanio yetu kama chama ni mradi ukamilike ili huduma kwa wananchi zianze mara moja, kwa sababu wakulima wanachotegemea wao ni kilimo, kilimo kikiwa vizuri maisha yao yanakuwa bora,” amesisitiza Kihongosi.

Ameongeza kuwa mradi huo utasaidia kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji na kuwawezesha wakulima kuzalisha mazao kwa kipindi chote cha mwaka badala ya kutegemea mvua pekee, hatua itakayochochea ongezeko la kipato chao na kuongeza tija katika kilimo.

Awali, akisoma taarifa ya mradi huo Mhandisi Mkazi wa Umwagiliaji wa Wilaya, Gerald Kapukutu amesema mradi huo una thamani ya zaidi ya Sh bilioni 23.9, ukiwa na lengo la kuongeza eneo la umwagiliaji kutoka hekta 150 hadi hekta 1,700.

Amesema mradi unaotekelezwa na kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation unatarajiwa kunufaisha moja kwa moja wakulima 1,129 kutoka vijiji vya Mtandika, Msosa na Ruaha mbuyuni, huku zaidi ya wananchi 38,824 ni wanufaika wasio wa moja kwa moja.

Amesema utekelezwaji wa mradi ni asilimia 13, akifafanua sababu za kuchelewa kwa utekelezwaji zikiwa ni pamoja na mvua, kupanda kwa bei za mafuta kutokana na mgogori wa mashariki ya kati, uchelewa kwa malipo ya mkandarasi na uwepo wa mazao kwenye shoroba za mifereji.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button