Tiseza simamieni kongani BuzwagI

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeelekeza Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji kuhakikisha Kongani Maalumu ya Uwekezaji ya Buzwagi (BSEZ) inakabidhiwa kwa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) ili isimamiwe ipasavyo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Damas Ndumbaro, amesema uamuzi huo umetokana na tathmini ya kamati iliyobaini kuwa TISEZA ina uwezo mkubwa wa kuendeleza kongani hiyo kuliko kuiachia Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.
Amesema wakati wa ziara ya kamati katika eneo hilo walijionea uwepo wa miundombinu muhimu ikiwamo maji, barabara na umeme wa uhakika ambayo ni vivutio muhimu kwa wawekezaji wa ndani na wa nje. SOMA: Mpaka Tanzania na Kenya wawekwa alama
Ndumbaro ameeleza kuwa ni vyema Halmashauri ya Kahama ikaendelea kushughulikia majukumu mengine ya maendeleo ya wananchi, huku jukumu la kusimamia kongani hiyo likiachwa kwa TISEZA ili kuongeza kasi ya uwekezaji. Ameongeza kuwa kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), serikali ina wajibu wa kuendelea kuvutia wawekezaji ili kupunguza tatizo la ajira na kuongeza mapato ya taifa.
Kongani ya Barrick Buzwagi ina ukubwa wa hekta 1,333 na ipo katika eneo lililokuwa Mgodi wa Buzwagi. Hadi sasa wawekezaji 35 wameonyesha nia ya kuwekeza katika eneo hilo. Mwekezaji mmoja tayari ameanza uzalishaji wa vipuri na vifaa vya migodini, huku watano wakiwa katika hatua za kupata leseni na wengine 29 wakiwa katika hatua za awali za uwekezaji.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Dk Pius Chaya, amesema serikali itazingatia mapendekezo ya kamati hiyo ya kuikabidhi kongani hiyo kwa TISEZA ili isimamiwe kikamilifu. Aidha, ameipongeza kampuni ya Barrick kwa ushirikiano wake na serikali kupitia Kampuni ya Twiga Minerals katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kuahidi kuwa ushirikiano huo utaendelea ili kuongeza fursa za uwekezaji nchini.
Kwa upande wake, Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Buzwagi, Zonnastraal Mumbi, alisema kampuni ya Barrick itaendelea kushirikiana na serikali katika kuvutia wawekezaji kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji na kufuata viwango vya kimataifa katika mchakato wa ufungaji wa mgodi.
Ameeleza kuwa mchakato wa kufunga mgodi huo ulianza mwaka 2021 kwa kushirikiana na Tume ya Kitaifa ya Ufungaji Migodi, huku hatua ya kubadilisha eneo hilo kuwa kongani ya uwekezaji ikilenga kutumia vyema miundombinu iliyopo.
Naye Mhandisi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA), Magige Marwa, amesema mradi wa ujenzi wa chujio la maji la Mwendakulima unatarajiwa kukamilika Juni mwaka huu. Alisema mradi huo utaweza kuhudumia zaidi ya asilimia 66 ya wakazi wa Manispaa ya Kahama kwa kuzalisha lita milioni 10 za maji kwa siku.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com