Meli mpya Bandari ya Karema kuchochea ukuaji uchumi Katavi

KUKAMILIKA kwa ujenzi wa meli nne kubwa za mizigo katika Bandari ya Karema mkoani Katavi, kunatajwa kuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kwa wananchi wa mikoa inayozunguka Ziwa Tanganyika pamoja na taifa kwa ujumla.
Mradi huo ulioanza Aprili 2025 unatarajiwa kukamilika Julai 2026 ukiwa umefikia zaidi ya asilimia 95, huku meli zote zikiwa tayari majini katika hatua za mwisho za uhakiki kabla ya kuanza kutoa huduma.
Msimamizi Msaidizi wa Bandari ya Karema, Anthony Poyo alisema hatua hiyo itaimarisha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Burundi na Zambia.
Alisema meli hizo zitakuwa na uwezo wa kubeba hadi tani 8,000 kwa wakati mmoja, jambo litakaloongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo, ikiwemo madini kama lithium, shaba na dhahabu kutoka Manono nchini DRC kupitia bandari za Kalemie, Kigoma, Dar es Salaam na Tanga kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.
Poyo alibainisha kuwa mradi huo pia utatoa ajira kwa Watanzania, hususan mabaharia ambapo kila meli itahitaji angalau wafanyakazi 15, sambamba na kukuza shughuli za upakiaji na upakuaji mizigo, biashara ndogondogo na huduma bandarini.
Aidha, alieleza kuwa wakulima watanufaika kwa kupata masoko mapana ya mazao yao ndani na nje ya nchi, hali itakayoongeza kipato cha kaya na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile alisema serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya usafirishaji ikiwemo reli ya kati na reli ya kisasa (SGR) ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka Karema hadi Dar es Salaam.
Alisisitiza kuwa kukamilika kwa reli ya Tabora hadi Karema kutakuwa chachu ya maendeleo zaidi katika ukanda huo.
Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Ankola Shipyard Co. Ltd, Mohammed Chande alisema mradi huo umefungua fursa za ajira na kuwajengea vijana ujuzi, licha ya changamoto za hali ya hewa zilizojitokeza wakati wa utekelezaji.
Baadhi ya wananchi wa Karema wamepongeza uwekezaji huo wakisema utachochea biashara na kuboresha maisha yao, huku wakiiomba serikali kuharakisha ujenzi wa barabara ya Mpanda hadi Karema ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa mizigo.




I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
Follow Here …………… http://www.giftpay7.vip
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com