Mchechu asifu mafanikio kuongezeka uwekezaji

ARUSHA; MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu amesema kuwa katika miaka mitano iliyopita uwekezaji wa serikali katika kampuni  umeongezeka kutoka Sh bilioni 821 hadi kufikia Sh trilioni 3.6, huku gawio likiongezeka kwa asilimia 357 kutoka Sh bilioni 58 hadi Sh bilioni 266.

Mchechu amesema hayo Jijini Arusha kwenye mkutano wa wakurugenzi wa kampuni zenye hisa ndogo ukiwa na kauli mbiu kutoka ufuatiliaji wa kawaida hadi uongozi wa kimkakati unaotazama mbele na kuongeza kuwa mikakati endelevu ndio itakayobeba kampuni kusonga mbele zaidi.

Amesema  mkutano huo ambao umeanza kufanyika tangu mwaka 2024, umekuwa jukwaa muhimu kwa viongozi wa kampuni kujadili utawala, utendaji na mchango wao katika mageuzi ya uchumi wa Tanzania.

Amesema  taasisi zitakazojenga uwezo wa kujitazama mbele kuwa na ubunifu na wepesi wa kubadilika ndizo zitakazofanikiwa kukabiliana na mabadiliko na kuchangia maendeleo.

Mkutano wa MIF 2026 unahusisha washiriki takribani 200, wakiwemo wakurugenzi, wakurugenzi watendaji, watunga sera na wataalamu kutoka ndani na nje ya Tanzania, wakijadili namna ya kuboresha utendaji na utawala wa kampuni hiz,i ili ziweze kuchangia zaidi katika maendeleo endelevu ya taifa.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    Follow Here …………… http://www.giftpay7.vip

  2. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  3. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button