TFS yapanda miti sekondari Shinyanga

SHINYANGA: WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeeleza kupoteza hekta 4069 za misitu kwa mwaka Tanzania Bara huku wakielekeza kupanda miti ya aina mbalimbali 350 kwenye Shule ya Sekondari Wasichana Shinyanga

Ofisa Misitu Mwandamizi ambaye ni Mkuu wa Operesheni Kanda ya Magharibi, Shadrack Msilu amesema hayo leo katika kuazimisha siku ya misitu duniani na kampeni ya upandaji miti kitaifa huku akieleza tangu mwezi Novemba mwaka 2025 wamefanikiwa kupanda miti zaidi ya milioni mbili kote nchini.

Msilu amesema kanda ya Magharibi inajumlisha mikoa minne ya Katavi, Tabora, Kigoma na Shinyanga ambapo wamekuwa wakisimamia na kutoa elimu juu ya sheria za misitu na hewa ukaa kwa wananchi ikiwemo utunzaji wa mazingira nakupanda miti.

Ofisa Mwandamizi wa Uhifadhi wa Misitu Wilaya ya Shinyanga Fabian Balele amesema licha ya upandaji miti wameanzisha utalii wa mazingira kwenye eneo la Lubaga ambalo litakuwa rasmi kwa ikolojia ya mazingira ya picha na utolewaji wa elimu ya utunzaji wa mazingira.

Mgeni rasmi Katibu tawala Wilaya ya Shinyanga Said Kitinga kwa niaba ya Mkuu wa wilaya Julius Mtatiro amesema Miti imekuwa ikiendelea kupandwa kwani historia hapa nchini Mkoa wa Shinyanga ulikuwa na hali mbaya ya ukatwaji wa miti bila kuipanda ukitofautisha na hali ya sasa imepandwa na kuwa kijani.

“ Halmashauri zimekuwa na mpango wa upandaji miti kila Halmashauri kupanda Miti Milioni 1.5 ambayo ndiyo sera iliyopo na kila mwananchi mwenye kiwanja apande mti na wataalamu wawasaidie kuona aina ya udongo unaostahili kwa aina ya miti,”amesema Kitinga.

Mwenyekiti wa kuhifadhi Mazingira kutoka klabu ya shule ya Sekondari Wasichana Shinyanga Kabula Bundala amesema shule ina wanafunzi 859 kidato cha kwanza hadi kidato cha sita na tangu kuanzishwa kwake mwaka 2023 kulikuwa na mti mmoja tu.

“Wanafunzi mpaka sasa wamejitahidi kupanda miti 12,053 ya asili na kisasa kwa uwiano wa miti 14 kwa kila mwanafunzi baada ya kupatiwa miti hiyo na TFS ila changangamoto iliyopo shuleni hapa ni undongo kwenye eneo hilo siyo mzuri miti haistawi vizuri,”amesema Bundala.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button