Mwinyi afungua fursa sekta ya anga

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kuimarisha sekta ya usafiri wa anga pamoja na kuendeleza mageuzi ya kidijitali ili kuvutia uwekezaji na kukuza uchumi.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu Zanzibar alipokutana na uongozi wa Liaoning Fangda Group of Companies kutoka China, ulioongozwa na Mwenyekiti wake, Ao Xinhua. Katika mkutano huo, Rais Mwinyi amepongeza dhamira ya kampuni hiyo kushirikiana na Zanzibar katika sekta mbalimbali za uwekezaji na kuahidi ushirikiano wa karibu.

Amesema Zanzibar ina fursa kubwa katika sekta ya anga kutokana na nafasi yake ya kiutalii, na kuwahimiza wawekezaji kutumia fursa hizo kuwekeza katika miundombinu na huduma za usafiri wa anga.Wakati huo huo, Rais Mwinyi amekutana uongozi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA) ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Khamis Juma Khamis.
Ujumbe huo uliambatana na wataalamu wa teknolojia kutoka Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit (GIZ) ya Ujerumani, wanaoshirikiana na BPRA katika kuboresha mifumo ya usajili na huduma za kidigitali. SOMA: Zanzibar, Marekani kuimarisha ushirikiano




Start making cash right now… Get more time with your family by doing jobs that only require for you to have a computer and an internet access and you can have that at your home. Starvt bringing up to $18012 a month. I’ve started this job and I’ve never been happier and now I am sharing it with you, so you can try it too. You can check it out here…
HERE→→→→→ https://PayAtHome1.Com/