Fedha za SGR zaipa tuzo Tanzania

SERIKALI ya Tanzania imeibuka mshindi wa tuzo ya kimataifa ya fedha za miundombinu kwa mwaka 2026, kufuatia mafanikio yake katika kupata mkopo wa masharti nafuu kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Umeme (SGR).
Tuzo hiyo ilitolewa kutokana na upatikanaji wa mkopo wa dola za Marekani bilioni 1.78 utakaotumika kugharimia ujenzi wa awamu ya tatu na ya nne ya mradi wa SGR. Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Rished Bade, alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya serikali katika hafla ya kimataifa ya tuzo za benki na masoko iliyofanyika jijini Cape Town, Afrika Kusini.
Ushindi huo unatokana na juhudi za Serikali katika kutafuta na kupata ufadhili wa mradi huo mkubwa wa kimkakati unaolenga kuimarisha uchumi wa nchi na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na abiria ndani ya Tanzania na katika Ukanda wa Maziwa Makuu. SOMA: Treni 5 SGR kubeba mizigo bandarini Dar kwa siku

Mkopo huo ulipatikana kupitia ushirikiano wa taasisi za bima kutoka Sweden, Poland na Italia pamoja na benki za maendeleo za kikanda, chini ya uratibu wa Benki ya Standard Chartered. Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Natu Mwamba, walisema kuwa mafanikio hayo yanatokana na uongozi thabiti wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kusimamia deni la taifa na kuhakikisha upatikanaji wa mikopo yenye masharti nafuu.
“Tuzo hii inaendelea kuiweka Tanzania katika nafasi nzuri kwenye masoko ya fedha ya kimataifa, na inaonesha uwezo wa nchi kupanga na kutekeleza mikataba mikubwa ya kifedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo,” alisema Balozi Omar.
Tuzo hizi za kimataifa zimekuwa zikitolewa tangu mwaka 2014 kwa lengo la kutambua nchi na taasisi zilizofanikiwa kuingia mikataba bora ya kifedha kupitia masoko ya mitaji na mikopo. Vigezo vinavyozingatiwa ni pamoja na ubunifu katika mipango ya kifedha, masharti nafuu ya mikopo na ubora wa utekelezaji wa miradi.
Mbali na ushindi huo, hivi karibuni Tanzania pia ilipata tuzo ya jumla ya mwaka katika usimamizi wa deni la umma kupitia Jumuiya ya Madola. Aidha, nchi ilishinda Tuzo ya Ofisi Bora Kanda ya Afrika kupitia Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali katika Wizara ya Fedha. Tuzo hizo zilitangazwa Machi 26, 2026, wakati wa mkutano wa Jukwaa la Jumuiya ya Madola kuhusu usimamizi wa deni la umma uliofanyika jijini London, Uingereza.




I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
This is what I do…… http://www.giftpay7.vip
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com