Lukuvi Atakumbukwa kwa Mengi

WAZIRI Mkuu Dk.Mwigulu Nchemba, amesema aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Mbunge wa Isimani,William Lukuvi, atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika utumishi wa umma.
Amesema hayo wakati akizungumza katika ibada ya mazishi iliyofanyika kijiji cha Idodi, wilayani Iringa, akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan. “Mchango wake katika Chama, Jimboni na Serikalini ulikuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi,” alisema. SOMA: Vangimembe Lukuvi: Jabali la Siasa Mbunge Mkongwe Aaga Dunia

Amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi iliyoanzishwa na marehemu, ikiwemo ujenzi wa barabara za lami katika maeneo ya Pawaga na Isimani. Naye Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, amesema kifo hicho ni pigo kubwa kwa Bunge kutokana na umahiri wa Lukuvi katika utendaji.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira amewataka vijana kuiga uongozi wake, akieleza alivyoanzia ngazi za chini hadi kufikia nafasi za juu serikalini. Marehemu Lukuvi alifariki Machi 25, 2026 alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa.





I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. the potential with this is endless…,
This is what I do……. http://www.giftpay7.vip