Vangimembe Lukuvi: Jabali la Siasa Mbunge Mkongwe Aaga Dunia

TANZANIA imepoteza mmoja wa wanasiasa wake wakongwe na waliolitumikia taifa kwa muda mrefu, William Vangimembe Lukuvi, aliyefariki dunia leo, Machi 25, 2026, katika Hospitali ya Dodoma. Kifo chake kimetangazwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kupitia tanzia kwa taifa, akimtaja Lukuvi kuwa kiongozi aliyelitumikia taifa kwa uaminifu, uzoefu na uzalendo wa hali ya juu.

Lukuvi alizaliwa Septemba 1, 1955, na amefariki akiwa na umri wa miaka 70. Ataendelea kukumbukwa katika historia ya siasa za Tanzania kama mbunge mkongwe zaidi katika Bunge la 13, akiwa ameanza kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Ismani tangu mwaka 1995.

Kwa zaidi ya miongo miwili, aliendelea kuaminiwa na wananchi wake kwa kuchaguliwa mara kadhaa mfululizo hali iliyomfanya kuwa miongoni mwa wabunge waliodumu kwa muda mrefu zaidi nchini. Kabla ya kuingia bungeni, Lukuvi alianza maisha yake ya kazi kama mwalimu chini ya Wizara ya Elimu kati ya mwaka 1975 hadi 1980. Baadaye aliingia kikamilifu katika siasa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), akihudumu katika nafasi mbalimbali za uongozi wa vijana kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa.

Aliwahi kuwa Katibu wa Vijana wa CCM katika ngazi ya mkoa na wilaya kati ya mwaka 1980 hadi 1984, na baadaye kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mwaka 1993 hadi 1994 nafasi iliyochochea safari yake kuelekea uongozi wa juu serikalini. SOMA: Waziri Lukuvi afariki dunia

Katika utumishi wake wa serikali, Lukuvi alishika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Naibu Waziri, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Dodoma pamoja na Uwaziri katika wizara tofauti. Alitambulika zaidi alipohudumu kama Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambapo alijijengea sifa ya kuwa kiongozi mwenye msimamo thabiti katika usimamizi wa ardhi na utawala bora. Aidha, hadi umauti wake alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu.

Kitaaluma, Lukuvi alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Kitanewa kuanzia mwaka 1962 hadi 1970, kabla ya kuhitimu Cheti cha Ualimu katika Chuo cha Ualimu Tabora mwaka 1975. Aliendelea kujiongezea elimu ya juu, akipata stashahada ya juu (Advanced Diploma) ya Sayansi ya Siasa katika Komsomol High School, Moscow nchini Urusi (1982–1983).

Mwaka 2001 alipata Shahada ya Kwanza ya Diplomasia na Masuala ya Kimataifa na baadaye Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kati ya mwaka 2008 hadi 2011 Mbali na elimu yake rasmi, alipitia pia mafunzo mbalimbali ya uongozi, ikiwa ni pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mafunzo ya kimataifa ya uchaguzi na bunge yaliyomjenga kuwa kiongozi mwenye uzoefu mpana wa kisiasa na kiutawala.

Kwa miongo kadhaa ya utumishi wake, Lukuvi alijijengea heshima ya kuitwa “jabali la siasa” kiongozi aliyesimama imara, aliyewatetea wananchi wake na nguzo muhimu katika utendaji wa serikali. Kifo chake kinaacha pengo kubwa katika siasa za Tanzania hususan kwa wabunge wakongwe na viongozi waliokuwa wakitegemea uzoefu wake ndani ya Bunge.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button