Jaji Chande: Tume iko huru

DAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa Tume ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, amesema tume hiyo ni huru na inajitegemea.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 8, 2026, Jaji Chande amesema tume ipo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha kazi, ikichambua ushahidi kwa kina kuhakikisha ripoti yake ina ubora unaotakiwa, na kwamba ripoti itatolewa kwa Kiswahili na tafsiri ya Kiingereza.

“Tume inajitegemea kwa kila kitu, Tume ndio mhariri, msahihishaji, na mamlaka iliyotupa kazi tunaonana nayo tu wakati tunapewa hadidu za rejea na wakati tunamkabidhi ripoti ya mwisho,”

“Hakuna mtu yeyote hapa katikati, hatuna dalali, tunafanya kazi yetu tumalizie na tupo katika hatua ya mwisho katika kutafsiri,” amesema Jaji Chande.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button