Wadau wakutana kujadili mkakati AFCON 2027

DAR ES SALAAM — Wadau kutoka taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi wamekutana kujadili Mkakati wa Kitaifa wa maandalizi ya Mashindano ya AFCON 2027, katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Johari Rotana na umewakutanisha wadau muhimu kwa lengo la kuweka mwelekeo wa pamoja wa maandalizi ya Tanzania katika kushiriki na kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa ya soka barani Afrika.

Majadiliano yamelenga kuimarisha uratibu, kuongeza ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi, pamoja na kubaini fursa za kiuchumi na kijamii zitakazotokana na mashindano hayo.

AFCON 2027 inatarajiwa kuwa moja ya matukio makubwa ya michezo barani Afrika, huku maandalizi yake yakihitaji mipango madhubuti katika miundombinu, huduma na usimamizi wa matukio.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button