Tanzania mambo safi tuzo za utalii duniani

DAR ES SALAAM: TANZANIA imeendelea kung’ara katika anga la kimataifa baada ya kuingiza vipengele 41 katika Tuzo za Utalii na Usafirishaji Duniani (World Travel Awards), hatua inayoimarisha nafasi yake kama moja ya vinara wa utalii barani Afrika.

Akizungumza, leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Paulina Mkama, amesema tuzo hizo zinahusisha jumla ya washindani 85 kutoka sekta za umma na binafsi, zikilenga kutambua na kusherehekea ubora wa huduma, kuhamasisha ushindani na kutoa fursa kwa wadau na watalii kupigia kura vivutio bora duniani.

Paulina ameeleza kuwa ushiriki wa Tanzania katika tuzo hizo ni fursa adhimu ya kuitangaza nchi kimataifa na kuiweka katika ramani ya dunia kama kitovu cha utalii.

Ameongeza kuwa taasisi za serikali, ikiwemo TFS na TAWA, zimefanikiwa kuwasilisha vivutio vyake katika kinyang’anyiro hicho.

Kwenye kinyang’anyiro hicho , Tanzania imewania nafasi katika vipengele mbalimbali barani Afrika, huku vivutio vikubwa kama Hifadhi ya Taifa ya Serengeti vikitajwa kuwania tuzo za juu. Aidha, katika baadhi ya vipengele, washindani saba kati ya 14 wanatoka Tanzania, hali inayoonesha uimara na ushindani wa sekta ya utalii nchini.

Amebainisha kuwa sekta ya utalii inachangia zaidi ya ajira milioni moja kila mwaka, na mafanikio katika tuzo hizi yataongeza fursa za uwekezaji, ajira pamoja na kukuza pato la taifa.

Kwa sasa, kampeni ya “Kura Moja, Tiketi Moja kwa Tanzania” inaendelea, huku Watanzania na wadau wa utalii wakihamasishwa kushiriki kikamilifu kupigia kura nchi ili kuongeza nafasi ya ushindi.

“Mbali na kuimarisha ushindani wa ubora wa huduma, tuzo hizo pia huchochea ukuaji wa sekta ya utalii kupitia ubunifu, uwekezaji na kuongeza mvuto wa vivutio katika soko la kimataifa,” amesema Paulina.

Ameongeza kuwa kwa mara ya kwanza, baadhi ya vivutio vinavyosimamiwa na taasisi za serikali kama TAWA na TFS ikiwemo Mpanga Kipengere, Aman Forest Reserve, Selous Game Reserve, Pugu Kazimzumbwi na Kilwa Kisiwani, vimeingia kwenye ushindani huo, jambo linaloashiria kukua kwa sekta ya utalii nchini.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

  2. I get paid over $130 1 to 3 hours working from home with 2 kids at home. I never thought I’d be able to do it but my best friend earns over $27k a month doing this and she convinced me to try. The potential with this is endless.
    Heress——-> http://www.giftpay7.vip

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button