Mbunge ataka internship ipanuliwe

MBUNGE wa Viti Maalumu, Selina Kingalame, ameishauri Serikali kuanzisha mfumo wa elimu kwa vitendo (internship) kwa kada mbalimbali za elimu, kama ilivyo kwa taaluma ya utabibu. Amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza changamoto ya ajira kwa wahitimu wengi, kwani uzoefu wa kazi umekuwa kigezo muhimu kinachotumika wakati wa kuomba ajira.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma leo Aprili 14, 2026, wakati wa kipindi cha maswali na majibu, akibainisha kuwa wahitimu wengi hukosa ajira kutokana na kukosa uzoefu wa kazi unaohitajika. “Katika ajira nyingi zinazotangazwa, kigezo cha uzoefu kazini kimekuwa kikiathiri wahitimu wengi kwa kushindwa kukidhi sifa hiyo,” alisema.

Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Ameir, alisema Serikali inatambua umuhimu wa mafunzo kwa vitendo katika kuongeza ubora wa wahitimu. Amefafanua kuwa kwa sasa Serikali, kupitia vyuo vya kati na elimu ya juu, tayari imeweka utaratibu wa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi, ingawa utekelezaji wake hutofautiana kulingana na kada na mahitaji ya taaluma husika.

Aidha, amesema Serikali inaendelea kuboresha miongozo ya mafunzo hayo ili kuongeza tija na kuhakikisha yanaendana na mahitaji ya soko la ajira. Ametolea mfano kada ya ualimu, ambapo Serikali imeandaa Kiunzi cha Kitaifa cha Mafunzo ya Ualimu kwa Vitendo cha mwaka 2026, kitakachotekelezwa kwa mtindo unaofanana na ule wa taaluma ya utabibu.

Mpango huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa rasmi katika mwaka wa masomo 2026/2027, hatua inayotarajiwa kuongeza ujuzi wa vitendo kwa wahitimu na kuwapa ushindani zaidi katika soko la ajira.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. thisis a fantastic article, really nice created, i enjoy reading it, i will be back to check out for latest update, keep up the good work and applause. ng.yandaz.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button