Shule binafsi zafundwa elimu bora

KAGERA: Ofisa Elimu wa Sekondari Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, Wandera Rwakatare ametoa wito Kwa wawekezaji wa shule binafsi kupunguza vita ya kuchonganishana kuzua taarifa za uongo badala yake wajikite kutoa elimu bora yenye ushindani ili kupata wanafunzi wengi

Kupitia mahafari ya 14 ya kidato cha sita ambayo yalifanyika Katika Shule ya Ushirika wa wakulima wa kahawa Karagwe na Kyerwa KDCU alisema kuwa amekuwa akisikitishwa na taarifa zinazoleta taharuki.

Alisema ni vyema wawekezaji wa maswala ya elimu watambue kuwa elimu inayovutia ni Ile inayoleta nidhamu wa watoto ,ushindi,mazingira bora ya kujifunzia ,uelewa wa viwango kwa watoto ,na sio taaarifa za kijipanga kusambaza uongo ambapo amedai kuwa wanaumisha taarifa za uongo na uvumishi hawatavumiliwa

“Nyaishozi Sekondari kwa miaka 6 Mfululizo imekuwa ikitokea nafasi za juu kitaifa katika mitihani ya kidato cha sita cha pili na cha nne ,na kutokana na ubora huo kumekuwa kuna taarifa mbaya ambazo mwanzoni zilituweka katika wasiwasi ila baada ya uchunguzi tumegundua kuwa ni vita ya kuharibiana ili kupata watoto ,sasa muda wa kufanya hiyo michezo utumike kuboresha shule na kupanga njia mpya za kuongeza maharifa kwa watoto”alisema Rwakatare.

Alisema ili kudhuitisha taarifa hizo alileta watoto kadhaa kusoma hapo ili kubaini yanayosemwa lakini ghafla hata watoto hao ambao hawakuwa na uelewa sana waligeuka lulu na kushinda na hawakuishia kushinda mienendo na Tabia zao zilibadilika kuwa njema zaidi jambo ambalo lilimvuatia pia kuhamisha mtoto wake Shinyanga na kumleta shuleni hapo ,ambapo ametoa nasaha ya wawekezaji kupendana na kushindana kukuza elimu ili kuvutia wazazi.

Alipongeza shule hiyo kwa namna inavyohakikisha watoto wengi wa wakulima wanaotoka wilaya za Karagwe na Kyerwa wanavyopata elimu bora na kusoma hadi elimu ya juu kwa lengo la kurudi kubadilisha jamii na kueneza kilimo cha sayansi kinachoendana na mabadiliko ya sasa.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Audax Gereon alisema kuwa shule hiyo unaendelea kutiiza Matakwa yake ya kutoa elimu Bora kwa watoto wa wakulima na watoto wote ambapo alisema kuwa kwa sasa shule hiyo inapokea watoto wote kutoka mikoa ya Tanzania.

Alisema kuwa kwa wale watoto ambao wazazi wao ni wakulima wa kahawa wanaendelea kukatwa Kidogo kidogo kwenye kahawa na watoto wao wakisoma bila kubuguziwa wala kuhojiwa

Alisema shule hiyo miaka 6 Mfululizo haijapata Daraja la tatu Wala la nne inapata Daraja la kwanza na la pili na sasa uongozi wa shule hiyo na wanafunzi wamekubariana kupata Daraja la kwanza pekee,huku akihaidi kuwa maadili na nidhamu ni kipaumbele cha kwanza katika shule hiyo ili kuleta matokeo mazuri

Baadhi ya wazazi walipogeza Elimu inayotolewa shuleni hapo huku wakidai kuwa watoto hao wanapokuwa katika mapumziko wamekuwa msaada mkubwa wa kutoa elimu ya kilimo cha kahawa katika familia zao na waliowazunguka kwani somo la kilimo katika shule hiyo ni la wote na halina ubaguzi .

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button