Mwasyoge: Michezo ni nguzo ya kuimarisha amani

MWENYEKITI wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), David Mwasyoge, amesema michezo ina nafasi kubwa katika kuimarisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Mwasyoge ameyasema hayo wakati akizungumza na Dailynews Digital kuhusu nafasi ya michezo katika amani ambapo amesema kuwa michezo hujenga mshikamano wa kijamii bila kujali tofauti za kidini, kisiasa au kikabila.

“Watu kutoka maeneo tofauti tumekutana kama familia moja. Kilichotuleta pamoja ni michezo ya kuogelea, na tunafanya kazi kwa pamoja. Umoja huu wa timu kwenye mchezo huu unanipa faraja kubwa,” amesema Mwasyoge.

Amesema kuwa umoja na mshikamano unaopatikana kupitia michezo unapaswa kuwa mfano kwa Watanzania wote, akihimiza jamii kujihusisha zaidi na michezo kama njia ya kudumisha amani na kuelewana. SOMA: Hans Rafael: Yanga SC ni imara licha ya majeruhi

“Michezo inawakutanisha watu wa aina mbalimbali, dini tofauti na itikadi tofauti, lakini wote wanakuwa na lengo moja. Hii ni njia nzuri ya kuimarisha amani na mshikamano katika jamii,” ameongeza.

 

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. In only 5 weeks, I worked parttime from my condo and acquired $30,030. In the wake of losing my past business, I immediately became depleted. Luckily, I found Sthis occupations on the web, and thus, I had the option to begin bringing in cash from home immediately. Anybody can achieve this tip top vocation and increment their web pay by:.
    Subsequent to perusing this article> w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

  2. Google pays $300 on a regular basis. My latest salary check was $8600 for working 10 hours a week on the internet. My younger sibling has been averaging $19k for the last few months, and he constantly works approximately 24 hours. I’m not sure how simple it was once I checked it out.

    This is my main
    concern…….w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button