Wizara yatakiwa kunufaika uzoefu wa mabalozi wastaafu

DAR ES SALAAM: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imetakiwa kutumia hazina ya maarifa na uzoefu kutoka kwa mabalozi wastaafu katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kuimarisha diplomasia ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo wakati akifungua kikao cha mashauriano kati ya uongozi wa wizara na mabalozi wastaafu kilichofanyika jijini Dar es Salaam Aprili 15, 2026.

“Wizara tumeanzisha utaratibu wa kuwa na vikao vya mara kwa mara na Mabalozi Wastaafu ili kuvuna maarifa na uzoefu wao kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia ili ulete nanufaa katika nyanja mbalimbali kama vile, siasa, ulinzi na usalama, uchumi, biashara, uwekezaji na utalii,” alisema Balozi Kombo.

Balozi Kombo ametaja mifano ya maeneo ambayo angependa Mabalozi Wastaafu wachangie maarifa na uzoefu walio kuwa nao ili maeneo hayo yaendelee kuwa na manufaa zaidi kwenye nchi.

Maeneo hayo ni pamoja na mwenendo wa ufanyaji wa biashara baina ya Tanzania na nchi nyingine, hususan zilizopo barani Afrika.

Utekelezaji wa Dira 2050 ambayo inalenga uchumi wa Dola bilioni 1, ni eneo lingine muhimu ambalo maarifa ya Mabalozi Wastaafu yanahitajika ili kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa wa ufanisi.

Waziri Kombo ameongeza kuwa mabadiliko yanayoendelea duniani
hususan, maendeleo ya kidigitali yanahitaji mikakati thabiti ili nchi iweze kunufaika na kuwa na mipango madhubuti ya kukabiliana na athari zake. Haya yote yanahitaji mawazo ya pamoja ili kuyaendeea kwa ufanisi.

Eneo lingine ambalo Waziri Kombo alisisitiza umuhimu wa kupata uzoefu wa Mabalozi Wastaafu ni siasa za ulimwengu ambazo zimekuwa hazitabiriki na zinasababisha madhara mbalimbali, hususan katika nchi zinazoendelea kama Tanzania.

Aidha, uzoefu wa Mabalozi Wastaafu unahitajika katika kuendeleza na kuimarisha taswira nzuri ya nchi na hasa nchi inapopewa dhamana ya majukumu ya kimataifa. Balozi Kombo alisema Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika mwaka 2028 na hivyo maarifa yao ni muhimu ili kuhakikisha nchi inatekeleza jukumu hilo kwa ufanisi.

Awali, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Dk Samwel Shelukindo alisema wizara inaangalia uwezekano wa kuanzisha utaratibu rasmi kupitia Ofisi ya Rais-UTUMISHI ili ushirikishwaji wa Mabalozi Wastaafu uwe unatambulika rasmi.

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she kaz convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website

    HERE——— http://www.giftpay7.vip

  2. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    HERE——————————————⊃⫸w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

  3. I create eighty five greenbacks every hour for operating a web job at . I ne’er thought I may have it off however my relief makes ten thousand bucks monthly working this job and she or he suggested Pine Tree State to be told additional regarding it. The potential with this can be endless.

    For more detail……. w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

  4. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button