Serikali, sekta binafsi kuendeleza ushirikiano

DAR ES SALAAM: MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema Serikali itaendelea kuunga mkono sekta binafsi kwani ina mchango kwa taifa kutokana na kwa sasa mawasiliano ni nyenzo muhimu baina ya wananchi na serikali.

Hayo ameyasema leo jijini Da es Salaam kwenye miaka 10 ya Kampuni ya NETIS inayohusika na ujenzi wa minara na kuhudumia pamoja na fiber ambapo amesema kampuni hiyo ina mchango mkubwa kwani imetoa ajira kwa vijana wa kitanzania na inaendana na dira 2050 kwa mawasiliano.
Kwa Upande wake, Happy Mushi Mkurugenzi wa Kampuni ya NETIS amesema wanajivunia kufikisha miaka 10 katika kukuza sekta ya Mawasiliano hivyo ameishukuru serikali na wateja wao katika kuhakikisha wanaboresha sekta hiyo.

Naye Vedastus Wembura mwakilishi kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema wizara inatambua mchango wao kwani imetoa ajira kwa wananchi hivyo ina tija na mchango kwa taifa.



