Mabalozi watakiwa kutangaza fursa za kibiashara

DAR ES SALAAM: Wizara ya Viwanda na Biashara imejipanga kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kibiashara na mabalozi wa Tanzania nje ya nchi ili kuhakikisha vikwazo vya kibiashara kimataifa vinaondolewa kwa wakati na ufanisi mkubwa na kuchochea ukuaji wa viwanda nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Waziri Salum amesema hayo Aprili 17, 2026, jijini Dar es Salaam alipofanya mkutano na mabalozi wateule watakaoiwakilisha Tanzania katika mataifa ya Jamhuri ya Korea, Comoro, Sweden, Saudi Arabia, Zambia, Oman, na Umoja wa Mataifa.

Aidha, Balozi Salum amesisitiza kuwa uhusiano imara wa kibiashara unategemea sana mawasiliano ya haraka ya taarifa na takwimu sahihi.

Vilevile amewashauri mabalozi hao kutangaza fursa za viwanda na biashara zilizopo nchini ili Tanzania inufaike kiuchumi kupitia wawakilishi wake waliopo nje ya nchi.

Kwa upande wao, Naibu Katibu Mkuu, Aristides Mbwasi, na Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Needpeace Wambuya, wameeleza kuwa ushirikiano huo ni msingi wa matokeo yanayoonekana, huku changamoto zikitafutiwa suluhu kupitia Kamati za Pamoja (JTC).

Pia Mabalozi wateule wameahidi ushirikiano wa dhati na kutoa ushauri wa kimkakati ili kuhakikisha biashara za Tanzania zinastawi katika masoko ya nje ya nchi.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

    This is what I do…. http://www.giftpay7.vip

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button