Viongozi wa dini, siasa waaga miili waliokufa mvua

KAGERA: Viongozi mbalimbali wa Serikali,siasa na dini wameungana na wananchi wa Kata ya Kibeta mtaa wa Anyama kushiriki Ibada ya kuaga miili ya watoto 2 kati ya 4 wa familia mbili waliokufa kutokana na mvua.

Mvua hiyo kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia Aprili 17 katika Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera, ambayo ilisababisha vifo vya watoto wanne.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima watoto wengine wawili ambao wamefariki katika tukio hilo tayari wamezikwa katika Kata ya Maruku Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.

Majina ya marehemu ni Eliza Edmundi miaka 13, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kashabo, darasa la sita, Edwini Edmund miaka 10, mwanafunzi wa darasa la nne Kashabo, Munihadi Mickidadi miaka 13.

Darasa la nne shule ya msingi Pamoja na Jamia ,Manihad mikdadi miaka mitano , lMiongoni mwa walioshiriki Ibada ya mazishi ni mbunge wa Jimbo la Bukoba Mwandisi Jonston Mtasingwa mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini ambaye alisema kuwa licha ya kuwa na majukumu ya vikao vya Bunge Jana alipata taarifa saa 12 asubh ambapo alituma msaada wa awali na mara baada ya kuuliza swali lake Bungeni alianza safari ya kurudi jimboni na alifika saa 6 usiku kuungana na familia hizo.

Aliiomba TANROAD na TARURA kuzibua mitaro hasa kipindi hiki cha mvua huku akiwataka wananchi kukagua nyumba zao mara kwa mara kwa kipindi hiki cha mvua.

Alitumia fursa hiyo kutoa pole kwa wananchi waliopoteza mifungo na makazi na kuomba waendelee kuchukua tahadhari kwani mvua Bado ni nyingi na nitaendelea kunyesha na kuomba wananchi kuendelea kushirikiana pale matatizo yanapojitokeza

Mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Sima alisema kuwa amesikitishwa na vifo hivyo abavyo vimekatiza ndoto za watoto wadogo ambao walikuwa na malengo makubwa ya baadaye.

Aidha alisema mvua hizo ambazo zimenyesha baadhi ya wananchi wamepoteza mifungo yao hasa kuku wengi wamesombwa na wanchi wengi wamepoteza makazi ambapo ametoa wito Kwa Wananchi wanaoishi mabondeni na kando kando ya ziwa Victoria kuchukua tahadhari kabla ya Vifo havijaongezeka.

Ibada ya kuaga miili hiyo imeongozwa na Mchungaji Ediso Rugemeleza Mchungaji wa Usharika wa kanisaa Kuu la Kiinjili la Kilutheri KKKT Dayosisi Kasikazini Magharibi.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button