Wiki ya Nishati yaanza Dodoma

DODOMA: Maonesho ya Wiki ya Nishati yanayohusisha Wizara ya Nishati na taasisi zake yameanza katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma huku yakilenga kutoa elimu ya nadharia na vitendo kuhusu Sekta ya Nishati.

Katika maonesho hayo wabunge na wananchi watafahamishwa kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya nishati kwa ujumla, ubadilishaji wa mfumo wa magari kwa ajili ya kutumia Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (CNG), masuala ya udhibiti pamoja na kujionea kwa vitendo matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Aidha, wabunge na wananchi watapata nafasi ya kufahamu hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya nishati na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali.

Maonesho hayo pia ni sehemu ya jukwaa la kubadilishana uzoefu na kupata mrejesho wa huduma zinazotolewa kwa wananchi ili kuendelea kuboresha huduma hizo na kuchochea maendeleo ya sekta nchini.

Taasisi zinazoshiriki maonesho hayo ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kampuni zake tanzu, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC) na kampuni zake tanzu.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Wakala wa Nishati Vijijini ( REA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli ( PURA) na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja ( PBPA).

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button