Wahitimu waahidi mapinduzi ya Sayansi

MANYARA: Uwekezaji wa serikali katika elimu kwa wanafunzi wasichana wa masomo ya sayansi mkoani Manyara umeelezwa kuongeza wataalamu wa sayansi nchini.
Jumla ya wanafunzi 104 wa Shule ya Wasichana Manyara wa masomo ya sayansi wamehitimu kidato cha sita.

Wameishukuruserikali kwa uwekezaji wa mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishia ikiwemo kukamilika kwa majengo ya shule yaliyogharimu Sh bilioni 4.5.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga, Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Fakii Lulandala, amesema shule hiyo ni kielelezo cha dhamira ya dhati ya serikali katika kuinua sekta ya elimu.

Aidha, amewasihi wahitimu kuepuka kufanya matendo maovu ikiwemo utumiaji wa dawa za kulevya, pombe au michezo ya kubahatisha .
Mkuu wa shule hiyo ya sekondari ya wasichana ya Manyara Gisela Msoffe,amesema shule ina jumla ya wanafunzi 510 na kuiomba Serikali kujenga uzio, kuongeza Matanki ya kuhifadhia maji.
Msoffe alibainisha mahafali hayo ya kwanza ya kidato cha sita yameongeza bidii ya kupenda masomo ya sayansi hasa kwa wasichana jamii ya watoto wa kifugaji.




https://shorturl.fm/MSZFm