Tanga kudhibiti wizi wa siafu, mayai ya bundi

SERIKALI mkoani Tanga kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), zitaendelea kuimarisha ulinzi wa pamoja katika Hifadhi ya Msitu ya Mazingira Asilia(RNFR) ili kudhibiti mienendo ya kuwepo wizi wa viumbe hai hususan siafu na mayai ya bundi.

Mkuu wa mkoa huo ,Balozi Bk Batilda Burian amesema  hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari pamoja na Maofisa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Ofisini kwake uu ya mkakati endelevu wa kuimarisha sekta ya utalii na utalii ikolojia  juzi.

“Tanga tunabahati kubwa ,Mwenyezi Mungu ametuneemesha kwenye utalii ,zipo hifadhi za kwanyamapori ,Mkomazi na Saadan  na pia hifadhi hizi za Msitu ya  Mazingira Asilia” amesema  Dk Burian.

Dk Burian amezitaja hifadhi hizo za  Msitu ya Mazingira Asilia ni pamoja Amani, Magamba na Nilo ambazo zipo katika jiografia ya ikolojia ya safu za milima ya Eastern Arc (Tao la Mashariki) zimekuwa na baadhi ya viumbe adimu na adhimu.

Amesema  hifadhi hizo zimekuwa  na viumbe adimu vikiwemo  vinyonga wenye mapembe matatu ,mapembe mbili  na pembe moja na pamoja na bundi ambao wanaopatikana Tanga na wengine Tao la Mashariki milima ya safu ya Uluguru Mkoani Morogoro.

“ Katika maeneo haya yanatembelewa na wageni wengi hasa watafiti wa ndani nan je ya nchi, wanafunzi kwa ajili ya kujifunza ya ikolojia ya viumbe hai“ alisema Dk Burian.

Dk Burian amesema  katika Hifadhi hizo , Serikali ya mkoa kwa kushirikiana na TFS wapo makini zaidi kubaini  watu wanaofanya wizi wa mayai ya bundi , viumbe vingine hai  hususani siafu.

“ Tuliona juzi kati kuna baadhi ya watu huko  waklishikwa wakiiba siafu, na sisi Serikali ya mko tumewaeeleza wenzetu wanaosimamia hifadhi hizi kwa maana ya TFS pamoja na wananchi kwa ujumla wawe makini kwa sababu kuna baadhi ya vitu sisi tunaona ni vya kawaida lakini vikishaondoka vitaleta athari kubwa sana “ amesema  Dk Burian.

Dk Burian amesema  siafu walikuwa wanapatikana sehemu nyingi duniani na kwamba baada ya maendeleo na shughuli zingine za ujenzi kwa sasa hawapatikaniki sehemu nyingi na kufanya watu kuja kuwatafuta maeneo kama hayo baadhi ya hifadhi .

“ Siafu wanafaida kubwa ya kutengeneza udongo , mbolea na vitu vingine , hivyo kwa sasa ni viumbe ambavyo tutaendelea kuvuilinda na ndiyo umuhimu wa hizi hifadhi za za  Msitu ya Mazingira Asilia” amesema Dk Burian.

Dk Burian amesema  uwepo wa  Hifadhi hizo zenye  vivutio vya kipekee ,mkoa umepanga kuongeza idadi ya watalii kutoka wastani wa 200,000 hadi kufikia 800,000 katika miaka michache ijayo.

Kwa upande wake Mhifadhi Daraja la kwanza wa TFS na Mkuu wa Hifadhi ya Msitu ya  Mazingira Asilia Amani, Nanzia Shedura amesema  hifadhi  hiyo  ipo katika Milima ya Usambara Mashariki .

Shedura alisema ni eneo muhimu la bayoanuwai lenye viumbe hai wa kipekee, wakiwemo spishi nyingi zinazopatikana eneo hilo pekee  duniani, ni paradiso ya ndege, ikiwa na zaidi ya spishi 340, baadhi zikiwa ni Amani Sunbird ,Usambara Eagle-Owl  na Ua la kipekee linalojulikana kama “African Violet”, linalopatikanakatika eneo hilo pekee duniani.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button