WIMA yatoa tuzo za heshima kwa wanawake 30 Afrika

DAR ES SALAAM: KATIKA jitihada za kutambua na kuenzi mchango wa wanawake katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi barani Afrika, Shirika la Women in Management Africa (WIMA) limetoa tuzo za heshima kwa wanawake 30 waliobainika kufanya vizuri katika nyanja mbalimbali za utaalamu.

Hafla hiyo imefanyika Aprili 25, 2026 jijini Dar es Salaam, ikihusisha wadau kutoka nchi mbalimbali za Afrika, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwanzilishi wa WIMA, Dk. Naike Moshi, ameeleza lengo kuu la taasisi hiyo ni kuongeza mwonekano, utambuzi na uwezeshaji wa wanawake kufikia nafasi za juu za uongozi, huku akisisitiza kuwa tuzo hizo sio kwa ajili ya kusherehekea mafanikio pekee, bali pia ni fursa ya kutambua vikwazo vilivyovunjwa na njia zilizofunguliwa kwa wanawake wengine.

Aidha, amebainisha kuwa licha ya wanawake kushiriki kikamilifu katika uongozi wa biashara na taasisi, bado uwakilishi wao katika bodi na nafasi za juu za maamuzi uko chini ya asilimia 30, kiwango kinachoonesha changamoto ya ushirikishwaji. Pia amesisitiza umuhimu wa kuendelea kujenga mifumo jumuishi yenye fursa sawa kwa wote.

Kwa upande wake, Profesa Makene ameeleza uwezeshaji wa wanawake unahitaji mifumo thabiti, uwajibikaji na juhudi endelevu, na kwamba WIMA ina mchango mkubwa katika kujenga majukwaa ya wanawake, kukuza sauti zao na kubadili mifumo inayowakwamisha.

Ameongeza kuwa wanawake wengi bado wanakabiliwa na changamoto za upatikanaji wa mitaji, mitandao na mifumo ya kijamii, lakini wanaendelea kuonesha uwezo mkubwa wa uongozi na ubunifu, pia amewataka viongozi kutumia nafasi zao kuwawezesha wengine, kuwekeza katika ubunifu na kuhakikisha mifumo ya maamuzi inawakilisha jamii kwa usawa.

Akichangia mada kuhusu changamoto za uongozi kwa wanawake, Balozi John Olanga amesisitiza umuhimu wa mafanikio ya pamoja badala ya mafanikio binafsi, huku akieleza kuwa mafanikio ya kweli yanapatikana pale ambapo mafanikio ya mtu mmoja yanachangia kuinua wengine, na kutoa wito wa kujenga harakati ya pamoja ya kuwakomboa wanawake katika uongozi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Fortis Insurance Brokers Ltd, Mariam Shamo, aliyeshinda tuzo ya kiongozi bora mwanamke, ameishukuru WIMA kwa kutambua mchango wake, na kusema kuwa tuzo hiyo imempa motisha zaidi ya kuendelea kuwawezesha wanawake, akibainisha kuwa zaidi ya asilimia 90 ya wafanyakazi katika kampuni yake ni wanawake.

Miongoni mwa waliotunukiwa tuzo hizo ni pamoja na Latoya Martine (Msumbiji), Vanessa Anioti (Tanzania), Lucia Minde (Tanzania), Dk. Upendo Matotola (Tanzania), Sarah Kiteleja (Tanzania), Dk. Aikande Kwayu(Tanzania), Caroline Yumbe (Tanzania), Bahati Minja (Tanzania), Shalot Matula (Botswana), Vida Nasari (Tanzania), Neema Mgimba (Tanzania), Anna Mushi (Tanzania), Dk. Sekela Mwaigomole(Tanzania), Sarah Mohamed (Tanzania) na Pauline Kinjumu (Tanzania).

Tuzo hizo zinachukuliwa kama sehemu ya juhudi pana za kuimarisha usawa wa kijinsia katika uongozi, huku zikilenga kuongeza uwakilishi wa wanawake katika nafasi za juu za maamuzi barani Afrika.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Mình chơi thử bên CM88 qua link https://7796.cn.com/
    thấy khá ổn, giao diện mượt, load nhanh kể cả lúc cao điểm. Nạp rút cũng nhanh gọn, không bị delay như mấy bên khác. Anh em mới vào có thể test thử.

  2. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she kaz convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website

    HERE————— http://www.giftpay7.vip

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button