Washindi shindano la uchoraji wapewa zawadi

DAR ES SALAAM:BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limetoa zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji kwa vijana lijulikanalo kama BASATA Youth Painting Competition, likiwa na lengo la kukuza na kuendeleza sanaa ya uchoraji nchini.

Katika shindano hilo lililohitimishwa katika ukumbi wa Idara ya Sanaa Bunifu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mshindi wa kwanza Stanley Inocent Mwinuka aliibuka kinara na kujinyakulia zawadi ya Sh 500,000.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Crispine Patrick Mboya aliyepata shilingi 200,000, huku Kelvin Peter Malonji akishika nafasi ya tatu na kujishindia shilingi 100,000.

Akizungumza na HabariLeo wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Edward Buganga, amewapongeza washiriki wote kwa ubunifu mkubwa waliouonesha katika michoro yao.

Amesema kuwa michoro 25 iliyowasilishwa katika fainali hizo imeonesha maudhmu mbalimbali yenye tija kwa jamii, ikiwemo uzalendo, utalii pamoja na urithi wa mila na desturi, jambo linalodhihirisha nguvu ya sanaa katika kuelimisha na kuhamasisha jamii.

Buganga ameongeza kuwa sanaa ya uchoraji inaweza kutumika kama nyenzo muhimu ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, hasa kupitia matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii yenye maudhui ya ubora na mvuto.

Aidha, amewahimiza vijana kuendelea kuchangamkia fursa zinazotokana na sanaa, akibainisha kuwa licha ya kuwepo mshindi mmoja, washiriki wote wanastahili pongezi kutokana na ubunifu wao.

Aliwataka kutumia vipaji vyao kuonesha maendeleo ya nchi kwa njia zinazoendana na ukuaji wa teknolojia.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. [ JOIN US ] I get paid more than $90 to $300 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this I have earned easily $10k from this without having online working skills . Simply give it a shot on the accompanying site…
    .
    You can check more.======= http://www.giftpay7.vip

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button