Filamu kuelimisha jamii changamoto za tabianchi

DAR ES SALAAM: SHIRIKA la My Legacy limekutana na asasi za kiraia zinazoshughulika na masuala ya wanawake, watoto na makundi maalumu kwa lengo la kuutambulisha mradi wa Mialo ya Kijani unaolenga kupaza sauti za wanawake wanaokabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kupitia filamu.
Akizungumza wakati wa mkutano huo jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa shirika hilo, Fortunata Temu, alisema wanawake wamekuwa miongoni mwa makundi yanayoathirika zaidi na mabadiliko ya tabianchi kutokana na majukumu wanayobeba katika familia na jamii.
Alieleza wanawake ndio wanaohusika zaidi na shughuli zinazotegemea rasilimali za asili kama vile kutafuta maji, kuni na kuhakikisha upatikanaji wa chakula cha familia, hali inayowafanya kuwa mstari wa mbele kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Alisema athari hizo zinajumuisha ukosefu wa maji safi, ongezeko la magonjwa na hata kuongezeka kwa vitendo vya ukatili vinavyochochewa na mazingira magumu ya kiuchumi na kijamii.
“Ni lazima tukubali kwamba mabadiliko ya tabianchi ni ajenda mtambuka ambayo haikwepeki na inayohitaji kuangaliwa kwa upana wake, ikihusisha pia masuala ya kijinsia.
Tumekutana na asasi hizi kusikiliza maoni yao ni kwa namna gani tutafanikisha filamu hii itakayoonesha sauti za wanawake kuhusu namna wanavyokabiliana na athari za mabadiliko haya,” alisema Temu.

Alieleza mabadiliko ya tabianchi ni kitu ambacho kitaishi miongoni mwa watu na kwamba changamoto zake zitaendelea kukabili watu hivyo ni lazima kuwepo na mbinu za kuhimili hali hizo.
“Katika filamu ya Mialo ya Kijani wanawake ambao mara nyingi wanasahaulika, watapaza sauti zao wao wenyewe ni namna gani mabadiliko ya tabianchi yanawaathiri na njia wanazozitumia kuhimili njia hii itatoa hamasa kwa watu wengine kutosubiri msaada,” alisisitiza Temu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la Habitat for Humanity Tanzania, Magdalena George alisema mabadiliko ya tabianchi ni kitu ambacho hakikwepeki kwa sasa na kwamba waathirika wa kwanza ni wanawake na watoto.
Alisema kama jamii inapaswa kubuni mbinu mbalimbali za kuhimili mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo mafuriko na ukame.
“Kwa mfano Dodoma kuna ukame na njia ya kukabiliana nao ni kupitia kilimo cha kisasa cha umwagiliaji, tusiwaache wanawake wakaendelea kuteseka kwa sababu wao ndio wazalishaji wakubwa,” alieleza.
Alisisitiza mradi wa mialo ya kijani ni wa kibunifu hivyo kupitia sauti za wanawake, Tanzania nzima itajifunza namna ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.
Naye, Meneja Mradi wa Vijana Artwork, Mandolin Kahindi alisema mradi huo unatumia sanaa kama vile filamu na maigizo kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa mambo mtambuka ikiwemo mabadiliko ya tabianchi na uhimilivu, usawa wa kijinsia na uhuru wa vijana kutumia sanaa kujipatia kipato.
Alisema sanaa ni njia ya mawasiliano ambayo inawatumiaji wengi hususan vijana na kwamba kwa kupitia filamu jamii itapata ujumbe wa namna wanawake ambao wamekuwa waathirika wakuu wa mabadiliko ya tabianchi wakibuni mbinu mbalimbali za kustahimili mabadiliko hayo.




:* I’m Jane Smith and I’m 23 years old. I am an aspiring model who is at least 18 years old. I enjoy having my photo taken in the sun. Please rate my photographs using this link.
……………………………………….➤ https://datewithmehere10.netlify.app/
:* I’m Jane Smith and I’m 23 years old. I am an aspiring model who is at least 18 years old. I enjoy having my photo taken in the sun. Please rate my photographs using this link.
………………………………………➤ https://datewithmehere10.netlify.app/