Mwanzilishi wa CNN afariki dunia

MAREKANI — Mwanzilishi wa mtandao wa habari wa CNN, Ted Turner, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87, familia yake imethibitisha kupitia taarifa iliyotolewa na Turner Enterprises.
Turner, ambaye alijulikana kwa maamuzi yake ya ujasiri katika sekta ya habari, alianzisha CNN mwaka 1980 na kuifanya kuwa televisheni ya kwanza duniani kurusha habari saa 24 mfululizo, hatua iliyobadilisha mfumo wa habari za televisheni duniani.
Mbali na habari, Turner alijenga himaya kubwa ya vyombo vya habari iliyojumuisha vituo vya televisheni, michezo na burudani. Pia alikuwa mfadhili mkubwa wa shughuli za kibinadamu kupitia United Nations Foundation, mwanaharakati wa kupinga silaha za nyuklia na mtetezi wa mazingira.
Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa CNN Worldwide, Mark Thompson, alisema Turner alikuwa kiongozi jasiri aliyebadili historia ya habari duniani.
Turner pia alijulikana kwa mchango wake katika uhifadhi wa mazingira na kurejesha nyati pori katika maeneo ya magharibi mwa Marekani.
Alifariki akiwa ameacha watoto watano, wajukuu 14 na vitukuu wawili.




I’ve found that having a clear step-by-step process, like you’d expect from a robust Otel Programı, makes even complicated recipes feel manageable. It’s all about breaking it down, isn’t it? My grandmother swore by her meticulous recipe cards.