Serikali yasisitiza ushindani wa haki kwa wawekezaji

DAR ES SAAM: Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Aristides Mbwasi amesema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 asilimia 70 inategemea sekta binafsi ikiwemo wafanyabiashara na wawekezaji, hivyo Serikali itaendelea kuwaunga mkono ili kufikia lengo.

Mbwasi amezungumza hayo leo Mei 14 katika amefungua rasmi Kongamano la Sheria za Ushindani na Wawekezaji Tanzania lililoandaliwa na Tume ya Ushindani (FCC), likilenga kujadili nafasi ya sheria za ushindani katika kukuza uwekezaji, biashara na maendeleo ya uchumi nchini.

Mbwasi amesema kongamano hilo lina tija kwa kubadilishana mawazo na kupeana ushauri na namna watahakikisha mazingira ya biashara yatazingatia ushindani wa haki.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa sheria za ushindani zina mchango mkubwa katika kujenga uchumi wenye usawa kwa kuhakikisha wawekezaji na wafanyabiashara wanapata mazingira ya haki na yenye uwazi.

Kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya FCC, Mwebesa Law Group pamoja na Primerio ya Afrika Kusini, kampuni yenye uzoefu katika masuala ya sheria za ushindani barani Afrika.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani ((FCC) Khadija Ngasongwa amesema mkutano huo utaisaidia kukuza uchumi pamoja na kuweka mazingira rahisi na wezeshi na uwekezaji ikiwa wa nje na ndani ya Tanzania  kwani sekta ya ushindani inasaidia kuboresha mazingira kwa mlaji.

Kwa upande wa Mshirika Msimamizi na Mwanasheria wa Mwebesa Law Group, Cris Mwebesa amesema mkutano huo umewakutanisha nchi mbalimbali kwani masuala ya ushindani ni mtambuka hivyo itasaidia kwa mlaji na sharia.

Kongamano hilo litawakutanisha wadau mbalimbali kutoka serikalini, sekta binafsi, mamlaka za udhibiti pamoja na wawekezaji kujadili utekelezaji wa sheria za ushindani, mwenendo wa soko na mazingira rafiki ya biashara.

Kupitia kongamano hilo litatoa fursa kwa wadau kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto za kisheria pamoja na kuangalia namna bora ya kujenga mazingira ya ushindani wa haki yanayochochea uwekezaji na maendeleo ya uchumi nchini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button