Bunge SC yadhaminiwa vifaa vya michezo

DODOMA; Kampuni ya Smart Sports imedhamini vifaa vya michezo kwa timu ya Bunge SC ya michezo mbalimbali, ikiwa sehemu ya maandalizi ya mashindano mbalimbali ya michezo yakiwemo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

‎Akizungumza leo Mei 19, 2026 jijini Dodoma wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo, Mwenyekiti wa Bunge Bonanza, Rebeca Nsemwa ameishukuru kampuni hiyo kwa udhamini huo na kuomba wadhamini wengine wajitokeze.

‎‎Amesema wabunge hushiriki mashindano mbalimbali, hivyo vifaa hivyo vimefika wakati sahihi.

‎Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Smart Sports, George Wakuganda amesema mahitaji ya vifaa muhimu kwa sasa yamekidhiwa na kilichobaki ni wabunge kuhakikisha wanajiandaa vizuri kupitia mazoezi ya mara kwa mara na kwamba wamekabidhi vifaa kwa michezo yote rasmi ambayo timu yaBunge SC inacheza.


Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button