Viongozi watakiwa kutambua mamlaka ni ya muda

MANYARA: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa, Kenani Kihongosi amewataka viongozi wa chama na serikali kutambua kuwa mamlaka wanayopewa na wananchi ni dhamana ya muda ya kuwatumikia.

Kihongosi ameeleza hayo leo Juni 3,2026 alipotembelea na kuahiriki kikao katika Shina Namba Nane, Kata ya Mirerani, wilayani Simanjiro mkoani Manyara, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

Kihongosi amesema viongozi wote, kuanzia ngazi za mashina hadi viongozi wa kitaifa, wanapaswa kukumbuka kuwa heshima na nafasi walizonazo zinatokana na dhamana waliyopewa kupitia CCM na wananchi.

Amewasisitiza kuwa mamlaka hayo si tiketi ya kujiona wakubwa, kujivuna au kutumia vibaya nafasi walizopewa,
hivyo hawana budi kuonyesha unyenyekevu, uwajibikaji na uadilifu katika utendaji wao.

“Lazima tutambue kwamba hizi heshima tulizonazo ni kwa sababu ya Chama Cha Mapinduzi. Mimi, Mwenyekiti wa mkoa, Diwani, Mbunge au kiongozi yeyote yule, tunapata nafasi hizi kwa sababu ya chama, kikiondoa dhamana hiyo, kila mmoja wetu anarudi kuwa mwananchi wa kawaida,” ameeleza Kihongosi.

Amesema dhamana ya uongozi inapaswa kutafsiriwa kwa matokeo yanayoonekana kwa wananchi kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, utoaji wa huduma bora za kijamii na usimamizi mzuri wa rasilimali za umma.

“Tunachotakiwa kufanya ni kazi, wananchi wanahitaji maendeleo, wanahitaji maji, elimu, afya na miundombinu bora. Hiyo ndiyo dhamana tuliyopewa na wananchi na ndiyo inayopaswa kuwa kipimo cha uongozi wetu,” amesema.

Awali, akisoma ajenda ya kikao hicho Katibi wa Shina Namba Nane, Careen Joseph amesema shina hilo linajumla ya wanachama 50, wakati wanachama 23 wakiwa ni wanaune na 27 ni wanawake.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button