CCM: CSR isiwe hisani, Iwe wajibu kwa jamii

MANYARA: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wamiliki wa vitalu na kampuni zinazojihusisha na uchimbaji na biashara za madini wanakamilisha kikamilifu dhana ya uwajibikaji kwa jamii(CSR), kikisisitiza fedha hizo si hisani bali ni wajibu wa kisheria kwa wananchi.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi ametoa mwito huo leo alipotembelea Soko la Madini ya Tanzanite Murerani wilayani Simanjuro mkoani Manyara.

Kihongosi ameeleza kuwa CSR inapaswa kuwa sehemu ya moja kwa moja ya mfumo wa maendeleo ya maeneo ya migodi, ambapo wananchi wanapaswa kunufaika na rasilimali zinazopatikana katika maeneo yao kupitia miradi ya kijamii

“CSR si hisani, ni wajibu ni lazima jamii zinazozunguka migodi zinufaike moja kwa moja na rasilimali zilizopo katika maeneo yao,” amesisitiza Kihongosi.

Ameongeza kwa kitoa mwito wa kuongezwa kwa usimamizi na msukumo wa serikali katika kuhakikisha kampuni zote zinatimiza wajibu wao wa CSR bila kusuasua.

Amesisitiza kuwa viongozi wa maeneo husika wanapaswa kuwa karibu na utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha wananchi wanapata matokeo yanayotarajiwa.

Akisoma taarifa ya mradi huo Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Eng. Grace Munuo Halmashauri hiyo iliingia makubaliano ya kimkata baina Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kama mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa Jengo hilo wenye thamani ya Sh bilioni 5.4.

Amesema manufa aya mradi huo ni kwambaunatarajiwa kupunguza changamoto za biashara holela za madini na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya sekta hiyo muhimu, pia kuwa chachu kubwa ya mageuzi katika sekta ya madini ya Tanzanite.

Ofisa Madini Mkazi Mirerani (RMO), George Kaseza amesa kushirikiana na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), jengo hilo linaendesha minada rasmi ya madini na tayari minada kadhaa imefanyika na madini yenye thamani ya mamilioni kuuzwa.

Amesema dhamira kubwa ni kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara ya madini yake, huku ikiandaliwa pia minada ya kimataifa ili kuongeza ushindani na manufaa kwa wachimbaji, wafanyabiashara na taifa kwa ujumla.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button