CCM yaitaka TFS kurejesha pikipiki walizokamata

MANYARA: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewaelekeza Viongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Mkoa wa Manyara kuhakikisha pikipiki zilizokamatwa kutoka kwa wananchi zinarejeshwa mara moja kwa wahusika ambao wamenyang’anywa.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi ametoa maagizo hayo leo Juni Mosi, 2026 katija viwanja vya Shule ya Msingi Katesh, Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara alipokuwa akizungumza na kusikiliza kero za wananchi.

Kihongosi ameelekeza hayo akijibu kero iliyowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Hanang’, Asia Halamga kuhusu wananchi wake kunyanga’anywa pikipiki na TFS na kuto kuwarudishia pale wanapopeleka faini wanayitakiwa kulipa.

Asia amesema mmoja ya wananchi hao alinyanga’anywa pikipiki na kutakiw akulupa faini ya Sh 500,000 lakini alipopeleka aliambiwa pikipiki imetaifishwa na kila Mbunge alupoagiza kifuatilia aludai kuwa wamekuwa wakimzungusha.

Akitoa maagizo hayo Kihongosi amesema suala hilo la kukamata na kukaa na pikipiki za watu Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba alishakata, akisisitiza kuwa kama chama anaelekeza pikipiki irudishwe kwa muhusika kabla hajaondoka katika mkoa huo.

“Jambo lingine ni suala la TFS kuhusiana na kukamata pikipiki, kwanza mheshimiwa waziri mkuu alisema watu wasikamate pikipiki na hapa chama kinaelekeza watu wa TFS mkoa, hao watu warudishe pikipiki mara moja, waende wakamkabili mwenye nayo,” ameelekeza Kihongosi.

Kihongosi amerejerea maagizo yaliyotolewa na Dk Mwigulu Aprili 30, 2026 akiwa bungeni alipoliagiza Jeshi la Polisi kote nchini kuziachia pikipiki zinazoshikiliwa kwa makosa madogo ili wahusika waendelee kuzitumia kujipatia kipato na kutekeleza wajibu wao wa kulipa faini wanazodaiwa.

Pia Dk Mwigulu alisisitiza kuwa pikipiki zinazohusishwa na makosa makubwa tu yakiwemo ubakaji, unyang’anyi, usafirishaji wa dawa za kulevya na matumizi ya silaha ziendelee kushikiliwa hadi uchunguzi utakapokamilika.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button