Wakulima wa korosho waishukuru serikali uwezeshaji pembejeo

MTWARA: BAADHI ya Wakulima wa zao la Korosho katika kata ya Naliendele Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara wameishukuru serikali kwa kuendelea kuwaletea pembejeo za korosho bure ili kuwapunguzia gharama za uzalishaji.

Hayo yamejiri wakati wa zoezi la ugawaji wa pembejeo hizo za korosho lilipofanyika kwa wakulima wa zao hilo kwenye kata hiyo huku likiendelea katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Wakulima hao ni kutoka AMCOS ya Naliendele akiwemo Amina Hamisi wa mtaa wa mkunjanguo kwenye kata hiyo amesema serikali inafanya kazi kubwa kila mwaka kuwashika mkono kuhusu suala hilo la pembejeo zinazowawezesha kuzalisha kwa tija.

“Mimi shamba langu lina hekari nne na nusu ila kabla ya serikali kuanaza kutuletea hizi pembejeo bure nilikuwa nikiuza korosho natunza kiasi cha pesa kwa ajili ya kununua pembejeo ila sasa hivi siwazii kuhusu pembejeo kama hivi serikali inatuletea”amesema Amina

Amesema yeye amepatiwa chupa mbili za pembejeo hizo zitazomwezesha kuhudumia mikorosho yake ili izae vizuri azalishe kwa tija ambapo msimu uliyopita wa kilimo 2025/2026 alipata mavuno ya gunia moja na nusu na baada ya mauzo alipata zaidi ya Sh laki 4 na matarajio ya msimu huu mwaka 2026/ 2027 kuzalisha zaidi ya hapo.

Mkulima mwingine ni Mussa Ally ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa wa mkunjanguo amesema shamba lake lina ukubwa wa takribani hekari ishirini na sita hivyo utaratibu huo wa kuendelea kuwaletea pembejeo inamsaidia kuleta ufanishi wa uzalishaji.

“Kusema ukweli baadhi ya sisi wakulima huko nyumba hatukuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba baada ya kulipwa ela ya mauzo ya korosho kwahiyo baadhi yetu tulikuwa tunapitia changamoto kidogo katika upatikanaji wa pembejeo ila sasa hali ni mzuri kwahiyo na tunamuomba mama Samia huu utaratibu aendelee nao”amesema Mussa

Kwa upande wake Ofisa Kilimo kupitia Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora BBT kutoka Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Merick Jonas amesema zoezi hilo la ugawaji wa pembejeo linalolenga kuongeza tija na uzalishaji kwenye korosho linaendelea vizuri na mwitikio wa wakulima ni mzuri.

Ofisa Kilimo mwingine ni Emmanuel Venance kutoka kwenye manispaa hiyo, ameendelea kuwaomba wakulima hao kuzingatia elimu inayotolewa na wataalamu hao juu ya matumizi sahihi ya pembejeo na endapo watapata changamoto yeyote katika matumizi hayo watoe taarifa ili wakapatiwe msaada husika.

Aidha pembejeo hizo za korosho za ruzuku kutolewa bure kila mwaka na serikali ili kuwapunguzia wakulima hao gharama za uzalishaji na zinaanza kutolewa za maji kwa ajili ya kuuwa wadudu na magonjwa ya korosho.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..    https://www.work27.info

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button