Kihongosi: Tuwapinge wanaohamasisha chokochoko

ARUSHA: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi, amewataka Watanzania kuendelea kulinda uhuru, amani na utulivu wa nchi kwa kupinga hadharani watu wanaohamasisha chokochoko na vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa taifa.

Kihongosi ameeleza hayo leo Juni 6,2026 alipotembelea na kuzindua Shina la Wakereketwa wa Noah Saccos, katika Stendi Kuu ya Mabasi Arusha mkoani humo, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini.

Akizungumza katika uzinduzi huo Kihongosi amesema Tanzania imejengwa juu ya misingi ya umoja, mshikamano na amani iliyopatikana kwa juhudi za waasisi wa taifa, hivyo wananchi wanapaswa kuendelea kuithamini na kuilinda.

“Hakuna jambo baya kama kuwa mtumwa ndani ya mataifa ya watu. Uhuru tulionao leo hapa, tulinde na wale wanaohamasisha chokochoko tuwapinge hadharani,” amesema.

Kihongosi amewataka wananchi kutokubali kutumiwa na wanasiasa wanaowashawishi kushiriki vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha yao na usalama wa taifa, akieleza kuwa mara nyingi madhara huwapata waliotangulizwa mbele huku waliohamasisha wakibaki salama.

Amesema baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwatumia vijana kutekeleza ajenda zao bila kuzingatia athari zinazoweza kuwakumba, jambo ambalo linapaswa kukemewa na kukataliwa na jamii.

“Usitumike na wanasiasa kuhatarisha uhai wako, awatakusaidia, haki ya Mungu nawaambia leo, hata waliopata madhara wametelekezwa na hao wanasiasa waliowatuma,” amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button