Watakiwa kuondoa vikwazo vya ajira kwa wenye ulemavu

DAR ES SAAM: Shirikisho la Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kilimanjaro Blind Trust Africa imehimiza waajiri nchini kuwapa fursa za mafunzo na ajira vijana wenye ulemavu kwani wana uwezo mkubwa wakuchangia maendeleo ya taasisi na uchumi wa nchi iwapo wakipata nafasi sawa .

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam Mratibu wa Mradi wa Youth Employability Skills Training Program (Tuajirike ) Grace Kajange alipowakutanisha waajiri mbalimbali na washiriki wa mradi huo ambapo amesema wana Mradi ambapo umewawezesha vijana wenye ulemavu kupata ujuzi unaowawezesha kushindana na soko la ajira ili kuongeza nafasi zao za kuajiriwa.

“Tunawalenga wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya kati kila Lindi litakuwa na washiriki 20 na kwa jumla tutawafikia vijana 140 katika kipindichiki cha majaribio Washiriki wanapatiwa mafunzo ya miezi mitatu yanayojumuisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Uandishi wa Wasifu Kazi (CV) ,Stadi za Mawasiliano pamoja na maadili na mienendo ya kitaaluma mahali pa kazi”amesema Kajange

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kilimanjaro Blind Trust Africa Suparna Biswas amesema mkutano huo umewalete waajiri wenye nia ya kuajiri kwa usawa ili kuwafungulia milango vijana wenye Ulemavu kwenye jamii.

Naye, Mohamed Mwanabonde Mwanafunzi mwenye Ulemavu anayenufaika na Mradi huo amesema waajiri wamekuwa na hofu ya kuwaajiri wakiamini hawana uwezo kumbe wana uwezo hivyo wasisite kuwaajiri.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button